Timu ya Yanga SC leo imezinduka tena kwa kuwachabanga kwa
jumla ya mabao 5-1 timu ya JKT Ruvu, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa,
jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Yanga wakionekana kuwa wachache zaidi katika mchezo wa leo dhidi ya JKT Ruvu ambapo walishinda bao 5-1.
Katika mchezo huo, winga wa Yanga, Mrisho Ngassa alifunga
bao tatu kwa dakika ya 8, 15 na 48, wakati goli la nne la Yanga lilifungwa na
Didier Kavumbagu dakika ya 40, huku lile la tano likifungwa dakika ya 51 na Hussein
Javu, wakati bao la kufutia machozi la JKT likifungwa na Idd Mbaga dakika ya
83.
Mechi ilianza kwa kasi, ila JKT walipunguza umakini na kuwapa
nafasi Yanga kulishambulia lango lao mara nyingi na kufanikiwa kuibuka na
ushindi mnono ambao pia umeibua matumaini ya kutetea ubingwa wao.
No comments:
Post a Comment