Timu ya
Yanga leo imeshindwa kujibu kipigo cha mtani wake wa jadi, Simba, baada ya
kutoka sare ya bao 1-1, mechi iliyopigwa katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
Salaam.
Bao la Simba
lilipatikana katika dakika ya 75 kupitia kwa Haruna Chanongo wakati lile la
Yanga liliingia dakika ya 88 kupitia kwa Simon Msuva, katika mechi iliyokuwa na
vituko vya aina yake.
Katika mechi
hiyo iliyokuwa na msisimko wa aina yake, mlinda mlango wa Simba, Ivo Mapunda,
hatashindwa kuisahau baada ya taulo lake kuibua kizaa zaa na kulazimika kutupwa
nje na wachezaji wa Yanga, wakiongozwa na Khamis Kiiza.
Katika mechi
hiyo, Yanga ndio waliokuwa na shauku ya kushinda kutokana na kushika nafasi ya
pili katika msimamo wa Ligi, huku ikiwa na kumbukumbu ya kupigwa bao 3-1 katika
mechi ya mtani jembe iliyowaacha mashabiki wake njia panda.
Awali mpira
ulianza kwa kasi huku kila timu ikijipanga kushinda katika dakika za mwanzo za
mchezo huo. Timu ya Simba iliweza
kumiliki vyema dakika tano za kwanza, kabla ya Yanga kuzinduka na kujibu
mashambulizi ya mtani wake.
Katika mechi
nyingine, timu ya Azam iliibuna na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu, mechi
iliyopigwa katika Uwanja wa Chamazi, jijini Dar es Salaam, hivyo kumaliza bila
kufungwa sambamba na kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Bara, huku bao la pekee
likipatikana katika dakika ya 79 kupitia kwa Brian Umony.
Mkoani
Tanga, timu ya Kagera Sugar iliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Coastal Union ya mkoani humo, huku bao lao likipatikana
dakika ya 50
kupitia kwa Themi Felix, akitumia kazi nzuri ya Paul Ngwai.
No comments:
Post a Comment