Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MUUNGANIKO
wa vyama vya upinzani, Chadema, CUF na TLP wamepanga kuanza kufanya mikutano ya
kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali, ikiwamo Katiba Mpya. Muunganiko
huo uliopewa jina la UKAWA, utaanza kufanya mikutano yao Visiwani Zanzibar kuanzia
Jumamosi.
Baadhi ya wajumbe wa UKAWA wakijadiliana jambo Bungeni Dodoma. Wajumbe hawa walisusa na kutoka nje ya Bunge jana mjini Dodoma.
Mtu
wa karibu na mdau wa mambo ya kisiasa na mwelekeo wa Katiba Mpya, aliudokeza
mtandao huu kuwa dhamira ya UKAWA kufanya mikutano katika Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ni kuishtaki serikali ya CCM kwa wananchi, kwa madai wanataka
kupora haki ya Katiba.
Mikutano
hiyo itaanza kufanyika siku chache baada ya UKAWA kususa Bunge la Katiba
linaloendelea mjini Dodoma; jambo ambalo limeibua hisia tofauti kwa Watanzania.
“Hawa
jamaa wanataka kuzunguuka katika mikoa ya Tanzania Bara, wakianzia na Zanzibar
Jumamosi kwa ajili kuishtaki serikali ya CCM kwa madai kuwa inataka kuandika
Katiba ya CCM badala ya Watanzania wote,” alisema.
Taarifa
zaidi za mikutano ya UKAWA katika maeneo mbalimbali ya Tanzania zitaendelea
kukujia hatua kwa hatua.
No comments:
Post a Comment