Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Bunge la Katiba limeahirishwa hadi
Jumanne ya Agosti 5 mwaka 2014 kuendelea
na vikao vya kujadili Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bunge la
Maalum la Katiba limeahirishwa huku sura ya kwanza na sita ikiwa imeshika kasi kiasi cha kuibua mizozo iliyozalisha chuki kwa baadhi ya wajumbe.
Wajumbe wengi walionekana
kuvutana huku baadhi yao wakipinga serikali mbili wakitaka tatu na
wengine kusema serikali tatu ni mbaya zibaki mbili. Mvutano huo ulisababisha Wajumbe
wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kujitoa.
Akizungumza wakati anaahirishwa
Bunge hilo Maalum la Katiba leo mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel
Sitta, alisema kuwa wajumbe watakutana tena Agosti 5, mwaka 2014 kuanzia saa
tatu asubuhi.
Alisema kuwa wajumbe wengi
wameonyesha kufanya kazi nzuri kuchangia mijadala ya Katiba Mpya, ingawa changamoto
zilikuwa nyingi.
“Natangaza kuahirisha Bunge hili
nikiamini kuwa tutakutana tena kuendelea na vikao vyetu kwa ajili ya
kuitengeneza Katiba Mpya ya Watanzania,” alisema.
Awali wakati anachangia, Mjumbe
wa Bunge hilo, ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mizengo Pinda, alishangazwa na vijana wadogo kudharau kazi za waasisi wa Taifa
hili kwa kisingizio cha kutoa hoja ya Katiba Mpya.
No comments:
Post a Comment