Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA wa mchezo wa masumbwi wa klabu
ya Ashanti Boxing, yenye maskani yake Ilala, jijini Dar es Salaam, Rajabu
Mhamila ‘Super D’, amesema kwamba kufanyika kwa pambano la Erick Magana na
Mwaite Juma wilayani Chalinze ni sehemu ya kuendeleza mchezo huo na kuupatia
mafanikio.
Pambano hilo limepangwa kufanyika Aprili
15 katika Ukumbi wa Ndelema Inn, mjini Chalinze, ambalo halitakuwa la ubingwa,
huku ikiwa ni njia za kuweka harakati ya kuutangaza vizuri na kuurudisha kwenye
hadhi yake ya siku zote.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam juzi, Super D alisema kwamba wadau wa ngumi wamekuwa wakishirikiana
kwa mambo mengi, ikiwamo mbinu nzuri za kuuletea mafanikio makubwa mchezo wa
masumbwi.
Alisema mapambano kadhaa
ya utangulizi yatakuwapo likiwapo la Biglee Juma, Godfrey Sadick, Hussein
Pendeza nao wakitarajiwa kupanda ulingoni kwenye patashika hiyo itakayokuwa na
faida kubwa kwa wakazi wa Chalinze na Tanzania kwa ujumla.
“Tuna mipango kabambe ya
kutangaza mchezo wa masumbwi katika nchi yetu, hivyo tunaamini kwa pamoja
Chalinze watapata burudani kamili kutoka kwa vijana wao,” alisema.
Pambano limeandaliwa kwa
ajili ya kuhamasisha mchezo huo nchini, ambapo kwa siku hivi karibuni
unaonekana kusua sua, hivyo hizi ni juhudi za kuuweka juu,” alisema.
Mchezo wa masumbwi
umeendelea kuwekewa mikakati ya kuuweka kileleni baada ya kuonekana kuwa
umeanza kusua sua katika kona ya ngumi nchini.
No comments:
Post a Comment