NA KAMBI
MBWANA, DAR ES SALAAM
NASIKIA
eti wale watoto wa mitaani waliokusanywa na kuelekea nchini Brazil wamepongezwa
na serikali baada ya kunyakua Kombe la Dunia kwa watoto wanaoishi katika
mazingira magumu.
Baadhi ya wachezaji wa mitaani waliopata taji nchini Brazil.
Kama hivyo
ndivyo, basi sisi tuna moyo wa ujasiri sana. Kwa maana tumekubali kuwa suala la
watoto wa mitaani Tanzania limemea kiasi cha kukosa mbinu mbadala ya
kupambana nalo.
Hii ni
kazi kubwa. Tanzania nchi yenye wingi wa vipaji, tunahitaji kuwa na sera nzuri
kwa ajili ya kuendeleza michezo, kama kweli tunataka kupiga hatua.
Huo ndio
ukweli. Vinginevyo siwezi kuvumilia, kwasababu naona porojo, siasa, huku tukiwa
wepesi kutafuta maeneo ya kupigia picha.
Kwanini
nasema hivyo? Hata hawa watoto wa mitaani wanaopongezwa leo kwa kuchukua taji
hilo, baada ya mwezi mmoja pengine wakawa wamerudi mtaani kuendelea na maisha
yao magumu.
Mwakani
watachukuliwa wengine, ukizingatia kuwa ni wengi kuliko wale wanaoishi maisha
mazuri. Tukiendelea na mtindo huu, Watanzania hatutakuwa na
mafanikio
katika michezo zaidi ya kusubiria kuokoteza watoto na kuwasafirisha nchi za
wenzetu na kuwatelekeza wakirudi.
Ndio maana
nasema tunapaswa kubadilisha fikra zetu. Tuwe na mipango imara kama kweli
tunahitaji kusonga mbele.
Huo ndio
ukweli wa mambo. Hizi akili za kuwapigia makofi watoto wa mitaani waliokotezwa
na kusafirishwa tumezipata wapi?
Basi
wakisharudi wote wapelekwe shule au kuwekwa katika kituo kimoja cha michezo
waendelezwe na sio kuwekwa kama pambo.
Au sisi
tunaona sifa matatizo? Kumbe imekuwa kawaida sasa kujigamba kwa idadi kubwa ya
watoto wa mitaani? Inawezekana ninachokiwaza si kizuri kwa upande wako, ila
kiukweli siwezi kuvumilia.
Si ajabu
baada ya watoto hao kurudi Tanzania, wamepata sehemu ya kusema na kutucheka kwa
upumbavu wetu. Tunaelekea wapi Watanzania?
Makampuni
yaliyojaa, lakini hakuna mipango imara ya kuendeleza michezo. Zaidi ya hapo
tunasubiria kuokoteza watoto hao na baadaye kuwapongeza.
Hii si
sawa. Tubadilisheni fikra zetu kama kweli tunahitaji kusonga mbele, maana
juhudi za kupiga picha ni nyingi kuliko mikakati ya ufundi inayoweza kuinua
soka la Tanzania.
+255712053949
No comments:
Post a Comment