Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum
Mayanga ametangaza wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho
(Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya
kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi
Manula (Azam), Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadili Ali (Azam). Mabeki ni Abdi
Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam),
Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said
Moradi (Azam).
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Frank
Domayo (Yanga), Himid Mao (Azam) na Jonas Mkude (Simba).
Washambuliaji ni Athanas Mdamu
(Alliance), Haruna Chanongo (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam),
Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngasa (Yanga), Mwinyi Kazimoto
(Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
Wachezaji walioitwa kutoka katika
kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati;
Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). Walinzi wa
pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba)
na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili
(Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini
Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na
Chunga Said Zito (Manyara).
Washambuliaji ni Mohammed
Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman
Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji
wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian
(Mbeya).
Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.
No comments:
Post a Comment