Baadhi ya Watanzania Visiwani Zanzibar wakionyesha ishara ya kuhitaji serikali tatu leo mjini Zanzibar ikiwa ni siku moja baada ya serikali kupitia jeshi la Polisi kupiga marufuku mikutano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Yafuatayo ni maandishi ya Julius Mtatiro, Naibu Katibu Mkuu BARA wa CUF, ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Katiba aliyesusa na wenzake.....
CCM WASIONESHE UDHAIFU KWA PROPAGANDA ZA KITOTO NAMNA HII;
Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa zenye ukweli wowote.
Mhe Zitto hajawahi kufuatwa na viongozi kuombwa ashiriki ktk shughuli
za UKAWA. Na hadi sasa UKAWA haijatangaza shuguli zozote zile zaidi ya mkutano wa Zanzibar ambao pia polisi wamekataa usifanyike leo hadi mara nyingine.
Kwa bahati nzuri, wakati mhe. Zitto Z Kabwe
akichangia sura ya 1 na ya 6 bungeni, alionesha njia sahihi kwa taifa
na kwa asilimia mia moja aliunga mkono hoja za wananchi na hata
mapendekezo ya UKAWA.....Kwa mfano Zitto Kabwe alisema, "hoja ya
serikali tatu kuvunja muungano siyo ya kweli. Alisisitiza kuwa muungano
unaweza kuvunjika ndani ya serikali moja, mbili, tatu na hata tano"
Ujumbe wa UKAWA ni HIYARI. Ndiyo maana baadhi ya wajumbe kama ISACK
CHEYO wali-walk out pamoja na UKAWA bungeni lakini keshoye walirejea na
kuendelea na bunge.
Umoja huu unaheshimu haki wajibu na
maamuzi ya kila mtu. Msimamo wa UKAWA ni kulinda na kutetea rasimu ya
maoni iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa msingi wa kulinda
mamlaka na maoni ya wananchi.
Tutafanya kazi na mtu yeyote
ambaye anaamini yale tunayoyasimamia. Hatutamuomba mtu yeyote asiyeona
uzito wa hoja zetu atuunge mkono, badala yake tutaendelea kuwaheshimu
wote wanaotofautiana nasi kwa hoja huku tukiendelea kupigania kile
ambacho tunakiamini.
J. Mtatiro,
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA),
Zanzibar.
No comments:
Post a Comment