Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar
es Salaam (DRFA), kimetangaza timu tatu zilizofanikiwa kucheza Ligi ya Mabingwa
wa Mikoa baada ya kufanya vizuri katika Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es
Salaam iliyomalizika Jumapili iliyopita.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Afisa Habari wa DRFA, Mohamed Mharizo, alisema timu hizo ni Navy SC
ya Temeke iliyokua vinara baada ya kujizolea pointi 34 ikifuatiwa na
Abajalo ya Sinza iliyojikusanyia pointi 31 na Mshikamano ya Temeke iliyokua na
pointi 30.
“Ligi yetu naweza kusema ilikua bora
na yenye ushindani kwa sababu tulianza raundi ya kwanza tukiwa na timu 32 na
baadae zikabaki timu 16 ambazo katika hizo tatu ndio zimefanikiwa kuwakilisha
mkoa wetu wa Dar es Salaam katika Ligi ya Mabingwa wa mikoa inayotarajia kuanza
Aprili 20 mwaka huu.
“Kwa niaba ya uongozi wa DRFA,
tunazipongeza timu hizi na tunaamini kwa dhati kabisa kuwa zitatuwakilisha
vyema katika Ligi ya Mabingwa wa mikoa na hatimaye kufuzu kucheza Ligi Daraja
la Kwanza,” alisema Mharizo.
No comments:
Post a Comment