Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
CHAMA Cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
kimeipongeza timu ya Azam FC kwa kufanikiwa kwa mara ya kwanza kutwaa ubingwa
wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2013/2014.
Nyota wa Azam waliofanikisha ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.
Azam FC ilijihakikishia kutwaa ubingwa huo Jumapili baada ya
kuifunga timu ya Mbeya City mabao 2-1 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa
kwenye Uwanja wa Sokoine.
Ofisa Habari wa DRFA Mohamed Mharizo alisema jijini Dar es
Salaam leo mchana kuwa ubingwa huo wa Azam ni kielelzo cha kujituma kwao na kuwa na
ushirikiano na walistahili kutwaa taji hilo.
“Kwa niaba ya DRFA nachukua fursa hii kuwapongeza wachezaji,
benchi la ufundi na viongozi wa timu ya Azam FC kwa ujumla, kwa kufanikiwa
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Ni imani yetu DRFA kuwa timu hiyo itawakilisha vyema nchi
katika michuano ya Klabu Bingwa barani Afrika, tunawatakia kila la kheri katika
michuano hiyo.
“Lakini pia tunaipongeza Yanga kwa kushika nafasi ya pili
katika ligi hiyo, nao tunawatakia kila la kheri katika michuano ya Kombe la
Shirikisho. Sisi Mkoa tunafarijika sana kuona timu zetu za Mkoa wa Dar es
Salaam zinavyofanya vizuri,” alisema.
No comments:
Post a Comment