Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata maelezo
kutoka kwa Daktari wa Kituo cha Afya Inyonga Dk. Koni, Katibu Mkuu
alitembelea kituo hicho ambacho kimeombewa kibali cha kuwa Hospitali ya
wilaya tangia mwaka jana mwezi Februari lakini mpaka sasa maombi
hayajajibiwa wala mkaguzi kutoka Wizara ya Afya hajafika kituoni
hapo, kituo hicho ni kikubwa chenye vitanda 90 na uwezo wa kulaza
wagonjwa 60 kwa mara moja, kina majengo ya kutosha na vifaa vya kutosha
kuwa Hospitali ya wilaya.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya vifaa vipya
kabisa vya kituo hicho cha afya cha Inyonga wilayani Mlele ambacho
kinaomba kupatiwa hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu kuendesha Pikipiki ya
kubebea wagonjwa iliyopo kwenye kituo cha afya cha Inyonga, kupewa hadhi
kuwa hospitali ya wilaya hospitali hiyo itasaidia wananchi wengi wa
wilaya ya Mlele kupata huduma karibu badala ya kusafiri umbali mrefu
mpaka wilaya ya Mpanda,hasa kupunguza sana vifo vya Mama na Mtoto.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya
Inyonga wilaya ya Mlele mkoani Katavi na kuwapongeza kwa umahiri wao wa
kuchapa kazi na kuchangia maendeleo yao na alisisitiza kuwa kero
zinazowakabili za kupata hospitali ya wilaya, maji na umeme zitatuliwa
mapema.
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi wa kata ya Inyimbo katika viwanja vya shule ya msingi Inyimbo
No comments:
Post a Comment