Na Kambi Mbwana,
Dar es Salaam
LIGI ya
Tanzania Bara imemalizika juzi Jumamosi, ambapo Azam FC imefanikiwa kunyakua
taji kwa mara ya kwanza, ikiziacha Yanga na Simba zikibaki kujiuliza nini
tatizo?
Kikosi cha timu ya Mbeya City pichani.
Hii ni
kwasababu wao walionyesha shauku ya kulitwaa taji hilo, hata hivyo maandalizi
yao hayajakuwa ya uhakika. Kwa
kumalizika kwa ligi hiyo, ni maandalizi ya kuanza kwa ligi ijayo, huku timu
tatu zikifanikiwa kupanda daraja, jambo linalowapa fursa ya kushiriki Ligi
ijayo itakayokuwa na ushindani wa aina yake.
Timu
zilizopanda daraja msimu huu ni pamoja na Stand United ya Shinyanga, Ndanda FC
ya mkoani Mtwara na Polisi Morogoro. Timu hizi
msimu ujao zitashiriki Ligi Kuu, ambapo kwa sasa ni dhahiri wanapaswa kujiandaa
vizuri ili zionyeshe soka lao.
Hata
hivyo, ni wakati wa mashabiki wa soka katika mikoa ya Shinyanga, Mtwara na
Morogoro kuzithamini timu zao. Mashabiki
hawa wa soka waone namna ya kupanga muda wao kuzishangilia timu zao ili
zifanikiwe kucheza soka lao la haja.
Mashabiki
wa mkoani Mbeya waliweza kuonyesha uzalendo kwa timu yao ya Mbeya City kiasi
cha kuifanya kuonyesha cheche zao. Ingawa
mashabiki hawa walipunguza mapenzi kwa timu yao ilipofika timu ya Simba au
Yanga, lakini bado mashabiki hawa walionyesha shauku na mapenzi kwa timu yao.
Huu ndio
uzalendo unaotakiwa. Uzalendo huu ukiendelezwa, walau mafanikio yanaweza kuwa
makubwa kwa soka la Tanzania. Hakuna
haja ya kuzalisha timu za mikoani ambazo zinakutana na kasumba za Simba na Yanga.
Tunahitaji kuona watu wote wa mkoa wa Mtwara wanashirikiana kuibeba timu yao ya
Ndanda hata itakapotokea kucheza na Simba au Yanga.
Ukiacha
timu ya Polisi Morogoro, inayosimamiwa na Jeshi la Polisi, bado uzalendo ni
muhimu kwa timu zote za mikoani. Huu ndio
ukweli wa mambo. Kuna haja gani ya kuziacha yatima timu za mikoani? Ndugu zetu
wa Coastal Union ya Tanga, Mtibwa Sugar ya Turiani Mogorogo, Kagera Sugar ya
mjini Bukoba na timu nyingine zinahitaji ushirikiano wa wadau na mashabiki wa
soka wa mikoani kwao.
Kule Ulaya
ndio utaratibu wao. Timu za Manchester United, Arsenal, bado si sababu ya
mashabiki wa soka Uingereza kushindwa kuzithamini timu zao za Manchester City,
Chelsea na nyinginezo. Mtindo huo
unawapa faida kubwa. Soka lao linafanya vizuri. Watanzania ni wakati wetu
kujifunza na kuweka mikakati yenye kuibua chachu ya maendeleo yetu.
Ni ujinga
timu za mikoani kushindwa kufanya vizuri kwasababu ya uzalendo duni wa
mashabiki wa soka dhidi ya timu vigogo. Huu ni
wakati wa mabadiliko kwa mustakabali wa soka letu Tanzania. Tumeona mara kadhaa
timu zetu ndogo zikisua sua kwasababu ya watu kuweka macho yao kwa timu vigogo.
Hivyo
suala hili si zuri kwa maisha ya soka. Wakati tunazipongeza timu za Ndanda,
Polisi Morogoro na Stand United ya Shinyanga, ni wakati wetu kujua mbinu nzuri
za kuziendeleza timu hizi. Tuhamasishe
timu zetu. Tununuwe jezi na vifaa vyao vya michezo ili kutunisha pia mifuko
yao. Tunapoona wanaishi kwa kubangaiza, wale wenye uwezo wao wajitokeze
kunusuru ukata wao ili mambo yao yawe mazuri.
Tanzania
yetu ilivyo, mtu anaweza kutumia Milioni 50 kwa timu ya Simba au Yanga, wakati
timu yake ya mkoa inasua sua. Huu ni
ujinga wa karne. Na ndio maana tumeshuhudia Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed
Dewji ‘Mo’ akaishindwa timu ya African Lyon, hali ya kuwa bado anaisaidia klabu
ya Simba, licha ya timu hiyo kuwa ya kiubabaishaji.
Hili ni
jambo la ajabu kupita kiasi. Nadhani wakati huu tunazipongeza timu tatu
zilizopanda daraja msimu ujao, vyema wote tukafahamu kuwa tusipokuwa makini,
zitashuka daraja kabla hata ya kujiimarisha, ukizingatia kuwa Ligi ya Tanzania
Bara ina changamoto lukuki.
+255712053949
No comments:
Post a Comment