Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
KATIBU mwenezi wa tawi la Simba la TAZARA lenye maskani yake
jijini Dar es Salaam, Alfred Mdemu, amesema kwamba watawashawishi wanachama wao
wanaotokea katika tawi lao kujilinda na ununuaji wa vifaa vya michezo vyenye
nembo ya Simba ambayo ni batili.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mdemu alisema katika
kulifanyia kazi suala hilo, kila mwanachama wao lazima anunuwe vifaa hivyo
mahali panapojulikana au kuagizwa kwa pamoja kutoka sehemu husika.
Alisema kununua jezi ya Simba ambayo ni bandia hakuwezi
kuisaidia klabu hiyo kwakuwa fedha zao zinakwenda kwa wafanyabiashara wachache
wasiokuwa na malengo ya kuiletea mafanikio klabu yao hiyo yenye maskani yake
jijini Dar es Salaam.
“Kuanzishwa kwa matawi ya Simba kuende sambamba na
kufanikisha maendeleo kwa kuhakikisha kuwa wanachama wananunua vifaa halali vya
michezo, zikiwamo jezi ambazo timu nyingi ndio biashara halali.
“Kwa sisi TAZARA tunajipanga kuona namna gani tunanunua
vifaa halali tukiamini ndio klabu yetu itaingiza fedha nyingi badala ya kununua
kwa watu ambao sit u hawatambuliki, bali pia vifaa vyao vinakuwa vya bandia,”
alisema Mdemu.
Tawi la Simba TAZARA
lina wanachama 176, huku likiwa na mipango kabambe ya kuhakikisha kuwa ujio wao
huo unakuwa na tija kwa klabu yao inayoongozwa na Ismail Aden Rage kwa sasa.
No comments:
Post a Comment