Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa klabu ya Simba SC, umesema ingawa wapo kwenye nafasi ngumu kuwania
nafasi ya tatu ya msimu wa Ligi, ila wataendelea kujipinda hadi dakika ya mwisho,
ili waone wamevuna jambo gani kwa manufaa ya timu yao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Msemaji
wa Simba, Asha Muhaji, alisema bado hawajakata tamaa katika ligi ya Tanzania
Bara, ingawa bado hali imeendelea kuwa mbaya kwa upande wao.
Alisema benchi la ufundi na wachezaji wao wamekuwa wakifanya
bidii, ila matokeo mabaya hayawakatishi tamaa ya kuendelea kusaka heshima ya
klabu yao, ingawa alikiri kuwa mambo yatakuwa
magumu kutokana na ushindani uliopo katika kuelekea mwisho wa Ligi ya Tanzania
Bara, inayodhaminiwa na Vodacom Tanzania.
“Mechi yetu na Azam ilimalizika kwa kushuhudia tukifungwa
bao 2-1 ila bado hatujakata tamaa ya kuendelea kupigania nafasi za juu, ingawa
juu ya ubingwa inaonekana dhahiri kuwa tumejitoa katika mchakato huo,
“Lolote linaweza kutokea katika kuelekea mechi za mwisho za
ligi ya Tanzania Bara, hivyo naamini vijana wetu wataendelea kupigania heshima
ya timu yao ya
Simba,” alisema,
Kufanya vibaya kwa timu ya Simba, kumepokewa vibaya na
mashabiki wao, hali inayowafanya waelekeze nguvu zao kuishangilia Azam FC,
wakiwa na maana ya kuwabeba ili mtani wao wa jadi, Yanga asiweze kutwaa taji hilo.
No comments:
Post a Comment