Na Mwandishi Wetu, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula
pichani juu, amewataka wakuu wa wilaya mpya za Handeni na Lushoto mkoani hapa kuhakikisha
wanawajibika ipasavyo kwenye maeneo yao ikiwemo kuipatia ufumbuzi migogoro ya
ardhi na viwanja ambayo imeonekana kuleta manunguniko kwa wananchi.
Badala yake amewataka kuhakikisha
wanasimamia haki kwa usawa ili kuweza kuondoa migogoro hiyo kwenye maeneo
husika ikiwemo kuzipatia ufumbuzi changamoto nyengine ambazo.
Mkuu Mpya wa wilaya ya Handeni, Husna Rajab Msangi, Mkoani, akiapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Said Magalula. |
Alitoa wito huo jana wakati
akiwaapisha wakuu hao wa wilaya ya Handeni,Husna Rajabu na Mariam Juma wa Lushoto ambao
waliteulwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kushika nafasi hizo katika
halfa iliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
Alisema kuwa kimsingi wakuu hao
wapya wanapaswa kwenda kufanya kazi kubwa kwenye wilaya walizopangiwa ili
kuweza kuonyesha namna ya uwajibikaji wao katika jukumu hilo kubwa ambalo
walipewa na Mkuu wa nchi.
“Naombeni msimuangushe Rais akawa na maswali mengi kwa uteuzi aliowapa
hakikisheni mnatimiza majukumu yenu kwa kusimamia shughuli za maendeleo kwenye
wilaya zenu lengo likiwa kuzipa maendeleo “Alisema RC Magalula.
Aidha aliwataka kwenda kushirikiana
na wananchi katika maeneo wanayokuwa wakiongoza ili kuweza kuchangia harakati
za maendeleo kwa jamii zinazowazunguka.
Mkuu mpya wa wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Mariam Juma, akila kiapo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Magalula jana, |
Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka kuacha
kukaa maofisini badala yake watoke na kwenda kukaa vijijini ili kuweza kubaini
changamoto ambazo zinawakabili wananchi ili kuangalia namna ya kuzipatia
ufumbuzi.
Hata aliwataka waweke mikakati
mazuri ya kutenda haki kwa wananchi bila ubaguzi wa aina yoyote pamoja na
kuangalia jinsi ya kutatua migogoro iliyopo maeneo yao kwa kufuata sheria
zilizopo.
“Acheni kukaa maofisini kusubiria kuletewa taarifa badala yake tokeni
mkaangalie changamoto zinazowakabili wananchi lengo likiwa kuangalia namna ya
kuzipatia ufumbuzi haraka lakini pia jiepusheni na tabia ya umangi meza“Alisema
RC Magalula.
Awali akizungumza baada ya kuapisha
Mkuu Mpya wa wilaya ya Handeni,Husna Rajabu Msangi alisema kuwa atahakikisha
anatenda haki wakati akifuatilia na kushughulikia masuala ya migogoro ya ardhi
kwa kutafuta ukweli ili kuweza kutenda haki kwa kushirikiana na viongozi
wenzake.
No comments:
Post a Comment