Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Mwanza
MAUAJI ya albino yameendelea kushika kasi katika viunga mbalimbali vya nchi yetu, zaidi yakitokea pia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, kama vile Mwanza, Geita na maeneo ya jirani.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyir akizungumza na Ester Jonas, aliyelazwa Hospitali ya Bugando aliyejeruhiwa kufuatia tukio la uporwaji wa mtoto wake Yohana Bahati. Kulia kwa Mbunge ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, akiwa na watumishi wengine  wa taasisi hiyo jijini Mwanza.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaimar Kweigyri (katikati), akizungumza na binti aliyekutwa nyumbani kwa Ester Jonas, mama wa albino Pendo Bahati aliyeporwa na haijulikani alipokuwa. Kulia kwake ni Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services, Lugano Kasambala, aliyeambatana na mbunge huyo.

Kutokea kwa mauaji hayo si tu yanazua hofu kwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), bali pia huichafua nchi yetu inayoaminika Tanzania ni kisiwa cha amani kulinganisha na
nchi nyingine Barani Afrika.

Leo hii watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa na wasiwasi mkubwa wa uhai wao, licha ya kuwa na mapenzi makubwa na Taifa lao. Wakati hofu hiyo ikigubika nyuso za watu hao,

mashirika mbalimbali na viongozi wote wa serikali wamekuwa.

Miongoni mwa mashirika hayo ni Bayport Financial Services, taasisi ya kifedha inayojihusisha na mambo ya mikopo nchini Tanzania. Taasisi hii kwa kushirikiana na mbunge wa Viti Maalum, Al Sheimar Kweigyir, walifanya ziara katika Mkoa wa Mwanza, ili kujionea hali ya matukio ya ukatili kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.

Katika ziara hiyo, Bayport na Mbunge Shaimar walimtembelea Ester Jonas, mama wa Yohana Bahati anayepata matatibabu katika Hospitali ya Bugando, jijini Mwanza, kufuatia

kujeruhiwa na watu waliompora mtoto wake huyo na kusababisha kifo chake.

Aidha, Bayport pia walimtembelea Sofia Juma, mama wa Pendo Emmanuel, albino aliyetekwa mkoani Geita na hadi leo haijulikani kama yupo hai au amekufa, licha ya Jeshi la

Polisi kutangaza kuwashikilia baadhi ya watu waliodaiwa kuhusika na tukio hilo la uporaji wa mtoto.

Akizungumzia safari hiyo, Meneja Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, anasema kwamba wameguswa na kuumizwa na matukio ya mauaji ya albino yanayoendelea kutokea hapa nchini.



Anasema jambo hilo linaichafua nchi na kuondoa amani kwa watu wenye ulemavu wa ngozi, hali itakayowafanya waishi kwa mashaka makubwa katika nchi yao yenye amani ya utulivu.

“Bayport Financial Services tumeumizwa na matukio haya ya ndugu zetu albino kuuawa kila siku, tukiamini kuwa matukio hayo ya ukatili yanaondoa amani na albino wataishi kwa

mashaka.

“Tunaaomba Watanzania wote kwa kushirikiana na serikali na jeshi la Polisi tuhakikishe kwamba tunapambana na wote wanaofanya matukio haya yasiyostahili kuchekewa hata mara moja,” alisema.


Kasambala anasema albino ni watu kama wengine, hivyo wanaoamini kuwa wakiuawa au kutolewa viungo vyao vingine ni utajiri, wanajidanganya kwakuwa si kweli, zaidi

ya kuonyesha roho mbaya zisizofaa kuigwa na wote waungwana na wanaoishi kwa upendo.

Anasema kiungo chochote cha mtu mwenye ulemavu wa ngozi si utajiri, hivyo ni jukumu la kila mwana jamii kuhakikisha kwamba anatoa ulinzi kwa watu hao ili wapate haki yao ya

kuishi ambayo ni ya msingi. 

Kasambala ambaye ni Meneja Mauzo wa Bayport Kanda ya Ziwa kutoka Bayport Financial Services, taasisi inayojihusisha na mikopo anasema serikali iweke mikakati imara kuwakamata watu wote wanaofanya matukio hayo ya uhalifu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.


Kasambala akiwa na Mbunge Al Shaimar Kweigyir na baadhi ya watendaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, walishikwa na uchungu pale walipotembelea kwa wahusika walioondokewa na watoto wao, Pendo na Yohana, ambao kutoweka kwao kumeibua simanzi nzito.


Katika safari hizo, Bayport Financial Services iliandaa msafara wa mbunge huyo ambaye kimsingi ni balozi wa watu wenye ulemavu wa ngozi, kama alivyokuwa yeye, hivyo ziara

hiyo ilikuwa na faida kwao.

Kasambala alimhakikishia mbunge Al Shaimar Kweigyir kuwa malengo yao ni kuona mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanakoma, hivyo watatoa ushirikiano mkubwa ili kuona albino wanaishi kwa raha kama walivyokuwa Watanzania wengine.


“Inatia huruma kuona binadamu wenzetu wanaostahili kuishi kwa amani ili waitumikie nchi yetu na kukuza uchimi kwa ujumla wanatumia muda mwingi kuwaza namna gani wataishi

kutokana na matukio ya uhalifu dhidi yao yanayoendelea kutokea siku hadi siku.

“Naomba kwa pamoja tupambane na wahalifu hao hata kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi tunapohisi tofauti dhidi ya wageni au watu wanaojihusisha na matukio hayo kwa namna

yoyote ile,” alisema.

Katika safari hiyo, familia ya  Yohana na Pendo kila moja ilifarijiwa kwa kupewa kiasi cha Sh Milioni 2, ili ziweze kujiendesha baada ya kukumbwa na mkasa wa watoto wao

kutekwa na Yohana kufariki, huku Pendo akiwa hajulikani alipokuwa tangu alipotoweshwa.

Meneja huyo alisema safari yao si njia ya kuwapa furaha familia hiyo, ila kuhakikisha kuwa wanashirikiana nao kwa shida na raha, ukizingatia kuwa Bayport ni taasisi ya Watanzania wote.


Anasema endapo Yohana na Pendo wangekuwa salama, huenda wangekuwa wateja wao taasisi yao au hata kushirikiana nao kwa namna moja ama nyingine, jambo linaloonyesha kuwa wamedhulumiwa haki zao za msingi za kuishi kama inavyosema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Naye Mbunge Shaimar, aliishukuru Bayport Financial Services kuonyeshwa kuguswa juu ya matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayoendelea kutokea.


Anasema watu wanaofanya matukio hayo hawastahili kuishi katika nchi inayojipambanua kuwa ni ya amani na utulivu, hivyo kwa kushirikiana na wana jamii yote, wahakikishe kuwa

watu hao wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya kutoa haki.

“Watu wanauliwa kama wanyama ndani ya nchi yao, hivyo hali hii inasononesha wengi, akiwamo  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri

Mkuu Mizengo Pinda, ambao kwa pamoja wamekuwa wakihuzunishwa na matukio haya.

“Ni vyema serikali iendelee kupambana dhidi ya watu hao, huku wananchi wakitakiwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi la Polisi iwe njia rahisi za kuwabaini na kuwakamata watu

hao,” alisema.

Mbunge huyo aliwataka watu kutoa taarifa za wasiwasi kwa wanaotembelea kwenye maeneo yao au pia kuwataja wale wanaofanya vitendo hivyo vyua kuua watu wenye ulemavu wa

ngozi.

Anasema kwa nafasi yake amekuwa akilipigia kelele suala la mauaji ya albino bungeni, sanjari na kutafuta namna bora kuunganisha nguvu na wadau wote, zikiwamo taasisi, ikiwamo

Bayport Financial Services.

Mbali na hilo, pia mbunge huyo amekuwa akitoa mafuta maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi ili wamudu kuzilinda ngozi zao katika joto linaloweza kuwapa wakati

mgumu.

Shaimar alisema si kweli kama albino anaweza kumpa utajiri mtu mwingine kwa kuuawa kwake au kutoa kiungo chake, huku akisisitiza kuwa jamii iwalinde watu wenye ulemavu wa ngozi ili waishi kwa amani na kushiriki katika kazi zote za kujenga uchumi wao na nchi kwa ujumla.


Capt…..Bayport

One

Capt…..Bayport
two