Na Mwandishi Wetu, Burundi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya Jumatano, Machi 18, 2015 amewasili nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya Jumatano, Machi 18, 2015 amewasili nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini humo.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Maua kutoka kwa watoto waliokuja
kumlaki katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Bujumbura ambapo alianza
ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais
wa Burundi Pierre Nkurunzinza akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bujumbura leo jioni.Rais
Kikwete yupo nchini Burundi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo
anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Rais Kikwete ambaye amewasili Burundi akitokea Dodoma ambako alikuwa katika ziara ya kikazi pia leo Machi 19, 2015, atahutubia Bunge la Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki (EALA) katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) katika hotuba ya The State of the East African Community Address.
Saa chache baada ya kuwasili Bujumbura, Rais Kikwete amehudhuria chakula cha jioni ambacho ameandaliwa na Rais Nkurunzinza kwenye Hoteli ya Panoramique.
Wabunge wa Bunge la EALA pia wamehudhuria chakula hicho cha jioni.Rais Kikwete ataondoka Burundi mara baada ya kuhutubia EALA kurejea mjini Dodoma kuendelea na ziara yake.
Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakipokea heshima wakati nyimbo za Taifa za nchi zao zikipigwa
Rais Kikwete na mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakikagua gwaride liloandaliwa na jeshi la Burundi.
Rais Kikwete akiwa na Mwenyeji wake Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi jijini Bujumbura jana jioni.
Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment