https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, March 22, 2015

Afande Sele amfuata Zitto Kabwe ACT, aitosa Chadema

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI wa muziki wa Hip Hop nchini Tanzania, Selemani Msindi, Afande Sele, ametangaza kujiunga rasmi na Chama kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency, ikiwa ni saa chache baada ya Zitto Kabwe kujiunga nacho.
Mwimbaji wa Hip Hop Afande Sele akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati anatangaza kujiunga na ACT leo.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kwamba Sele aliyekuwa mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ameamua kujiunga na chama hicho ili aweze kutimiza azma yake ya kujihusisha na siasa kwa undani.

Sele alikuwa na lengo la kugombea Ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini mwaka huu, hivyo huenda ameamua kuhamia ACT  ili apate nguvu na ushawishi mkubwa wa kuweza kuwatumikia wana Morogoro kwenye uchaguzi huo.

Kuhamia kwa Sele ACT kunaongeza kasi ya joto la watu wanaoanza kukiangalia kwa jicho la matumaini makubwa chama hicho kilichoasisiwa kwa mlengo wenye dhamira ya kupambania sera zenye kuleta mustawi mpana wa maendeleo ya Tanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...