https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Saturday, February 28, 2015

John Komba afariki Dunia TMJ leo Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KIFO. Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni Mstaafu, John Komba, pichani, amefariki Dunia leo jioni katika Hospitali ya TMJ, sasa mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya jeshi la Lugalo. Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Marehemu Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa bendi ya TOT inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), amerafiki huku akiwa anategemewa kwa kiasi kikubwa katika suala zima la Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

Tayari Komba aliachia wimbo wake mpya uliokwenda kwa jina la CCM mbele kwa mbele, aliyouimba rasmi katika sherehe za kuzaliwa kwa CCM, zilizofanyika Songea mjini. Habari za kufariki kwa Komba zimepokewa kwa shingo upande na wadau wa CCM na Watanzania kwa ujumla.

Komba atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye chama hicho cha CCM kutokana na uwezo wake wa kutunga nyimbo za kampeni mara kwa mara ambapo nyimbo zake zimekuwa tegemeo kwa watu wote wanaofuatilia na wasiofuatilia siasa za Tanzania.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...