Na Mwandishi Wetu, Handeni
MIGOGORO kadhaa inayaoendelea kurindima katika kijiji cha
Misima, Kata ya Mabanda, wilayani Handeni, mkoani Tanga, imezidi kuipasua
kichwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athuman Malunda, pichani.
Jana mwenyekiti wa mtaa wa Kwedigondo, Idd Kisege alifikishwa
mahakama ya Mwanzo Handeni, kwa madai ya kuvamia shamba la Michael Panga (NADA),
wakati kesi kama hiyo inasikilizwa kwenye Baraza la Ardhi la wilaya Korogwe,
mkoani Tanga.
Mmoja wa waathirika wa migogoro Misima anayejulikana kwa jina la Idd Kisege, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Kwedigongo, kijiji cha Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga, akizungumza na wananchi wake hawapo pichani muda mchache baada ya kutoka mahakamani, akishtakiwa kwa kosa la kuigawa ardhi ya bwana Michael Panga (NADA).
Akizungumza mjini hapa, Mwenyekiti wa CCM Handeni, Athuman Malunda, alisema kwamba
Misima kuna matatizo mengi ambayo yanaashiria kuwa mitafaruku hiyo inaweza kuwa
mibaya kwa CCM.
Alisema kwamba miongoni mwa mitafaruku hiyo ni migogoro ya
ardhi inayoendelea kushamiri katika eneo hilo, likiwamo la NADA, ambaye
anaonyesha aliazimwa shamba hilo alime na serikal ya kijiji.
“Japo ipo migogoro mingine kama ile ya wananchi kugomea kuwa
kwenye Halmashauri ya Mji, lakini si suala kubwa isipokuwa hili la ardhi ambayo
kwa kipindi kirefu sasa imekuwa kero.
“Hata hivyo sisi kama chama tunaendelea kutafakari namna ya
kulifanyia kazi, ikiwamo kuwashauri au kuwasimamia watendaji wa serikali ambao
kimsingi wanapaswa kuwa makini katika ufuatiliaji wa suala hili,” alisema.
Misima ni sehemu pekee kwa wilaya ya Handeni ambapo katika
Uchaguzi wa Serikali za mitaa na vjjiji mwaka jana walionyesha kuwaangalia
wapinzani kwa mitaa kadhaa kuchukuliwa na Chama Cha Wananchi (CUF), ukiwamo
mtaa wa Kwedigongo.
No comments:
Post a Comment