Na Mwandishi
Wetu, Kwimba
TAASISI ya
kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo imepongezwa na serikali kwa hatua yake ya kufungua tawi wilayani
Kwimba mkoani Mwanza.
Meneja Mauzo
wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano
Kasambala, akimuelekeza jambo Katibu Tawala wa Wilaya Kwimba, Vicent Emmanuel,
katika uzinduzi wa tawi jipya wilayani humo, uliofanyika Machi 2 mwaka huu.
Wengine ni maofisa wa taasisi hiyo, Ramadhan Hanafi na Monica Mwangoka. Picha
na Mpigapicha Wetu.
Shughuli za
uzinduzi huo zilifanyika Machi 2 mwaka huu, huku mgeni rasmi akiwa ni Katibu
Tawala wa Wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, akiongozana na viongozi mbalimbali
wa serikali wilayani humo.
Katibu
Tawala wa wilaya ya Kwimba, Vicent Emmanuel, kushoto akikata utepe kuashiria
kuzindua rasmi tawi jipya la taasisi ya kifedha ya Bayport Financial Services,
wilayani Kwimba, mkoani Mwanza. Kulia ni Meneja Mauzo wa taasisi hiyo Kanda ya
Ziwa, Lugano Kasambala. Picha na Mpigapicha Wetu.
Akizungumza
katika uzinduzi huo, Katibu Tawala huyo wa wilaya Kwimba, Emmanuel alisema
kwamba kufunguliwa kwa tawi hilo kutatoa huduma karibu na wananchi, kama njia
ya kukuza uchumi wao kwa ujumla, zikiwapo fursa za kukopeshwa bidhaa
mbalimbali, vikiwamo vyombo vya usafiri.
Alisema
kwamba awali watu wa Kwimba walilazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma za
mikopo, lakini sasa wamesogezewa huduma karibu, hivyo ni jukumu lao kutumia
fursa hiyo kwa ajili ya kujinufaisha kwa ajili ya maisha yao.
“Serikali
tunaipongeza Bayport Financial Services kwa hatua ya kuanzisha tawi hapa
Kwimba, hivyo tunaamini kwa pamoja tutafanikisha maendeleo kwa watu wote kwa
kupitia njia ya mikopo kwa watumishi wa umma na wafanyakazi waliodhinishwa,”
alisema Emmanuel.
Naye Meneja
Mauzo wa Bayport Financial Services Kanda ya Ziwa, Lugano Kasambala, alisema
kwamba tawi lao limejipanga kutoa huduma bora kwa wakazi na wananchi wa Kwimba
waliokuwa wakisafiri umbali mrefu kupata huduma zao.
“Huu ni
mwendelezo wa Bayport Financial Services kuhakikisha kwamba tunaendelea
kufungua matawi katika sehemu mbalimbali, ambapo sasa tumefikisha matawi 79
nchini kote, ambapo uwapo wa taasisi yetu umerahisisha maisha kwa watumishi wa
umma na wafanyakazi waliodhinishwa na taasisi yetu.
“Tunaomba
wachangie fursa za mikopo mbalimbali kama ile ya bidhaa, mikopo ya fedha, bima
ya elimu kwa uwapendao, ambapo katika mikopo ya bidhaa, mteja anaweza
kukopeshwa bodaboda, vifaa vya ujenzi, injini za boti, pembejeo za kilimo na
huduma nyingine nzuri na muhimu kwa Watanzania wote,” alisema.
Kwa mujibu
wa Kasambala, huduma za Bayport ni rahisi kupatikana ndani ya saa 24, huku
zikiwa hazina amana wala dhamana, jambo linaloonyesha mafanikio makubwa kwa
wateja wetu watakaoamua kupata huduma katika taasisi yao.
Bayport
Financial Services ni taasisi inayojihusisha na mikopo, huku ikiwa na matawi
katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, ambapo kwa kupitia tawi la Kwimba, wateja
wao hawatalazimika kusafiri ili wapate huduma za taasisi hiyo.
No comments:
Post a Comment