Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
ALIYEKUWA Mbunge Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo Chadema Zitto Kabwe, amejiunga rasmi kwenye Chama chake
kipya kinachojulikana kama Alliance for Change and Transparency ( ACT),
imefahamika.
Zitto Kabwe kushoto baada ya kusaini kujiunga rasmi kwenye chama cha ACT usiku wa kuamkia leo, jjini Dar es Salaam. Picha kwa hisani yaa mitandao.
Habari zlizoanza kuenea katika mitandao ya kijamii na kwa
mtu wa karibu zilisema tamko la kuhamia kwenye chama hicho kipya atazitoa leo
saa tano asubuhi, jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kabla ya kukutana na waandishi wa habari, tayari
picha zake zimeanza kuzagaa katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha wakati
anasaini juu ya kujiunga kwenye chama hicho kinachotarajia kuingia kwenye
Uchaguzi wa ndani hivi karibuni.
Duru za siasa zinasema endapo Zitto asingeweza kujiunga na
chama hicho kipya jana, basi asingekuwa na sifa ya kugombea uongozi wowote
ndani ya ACT, inayotaka mwanachama wake aliyejiunga siku saba kabla ya uchaguzi
wao.
Hata hivyo juu ya
mwelekeo wake kisiasa na namna gani anaweza kuendelea kuwatumikia Watanzania
kwa mambo mbalimbali, Zitto ataongea mengi katikaa mkutano huo na waandishi wa
habari, ikiwa ni siku moja baada ya kuachia ngazi rasmi kwa kuaga bungeni.
No comments:
Post a Comment