Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile (katikati)
akiwasili katika ukumbi wa mikutano kwenye hoteli ya Hyatt Regency akiwa
ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi
na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia) pamoja na Mratibu Mkazi
wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez kwa ajili ya
kuzindua rasmi ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, uzinduzi
uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Nyuma yao
ni Mkurugenzi wa Programu kutoka Taasisi ya Uchumi na Utafiti wa Kijamii
nchini (ESRF), Dk. Tausi Kida.
Na Mwandishi wetu
UMOJA
wa Mataifa umesema kwamba utaendelea kuisaidia serikali ya Tanzania
katika kutanzua changamoto za maendeleo zinazoikumba nchi hii.
Kauli
hiyo imetolewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja huo (UNDP), Alvaro
Rodgriguez wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya maendeleo ya Binadamu ya
mwaka 2014 mwishoni mwa wiki.
Ripoti
hiyo imeandaliwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na jamii-
ya ESRF kwa ufadhili wa UNDP na inagusia changamoto za Maendeleo .
Katika
hotuba yake amesema kwamba Umoja wa Mataifa unaona juhudi za serikali
katika kuwakwamua wananchi katika umaskini na kutokana na hali hiyo
wataendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo pamoja na utafiti
wenye kulenga kutoa suluhu kwa changamoto za maendeleo ya wananchi.
Mshehereshaji
wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania, Taji
Liundi akiitambulisha meza kuu kwa wageni waalikwa (hawapo pichani)
waliohudhuria uzinduzi huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Ripoti
hiyo ambayo inazungumza: "mabadiliko ya kiuchumi kwa maendeleo ya watu"
imesheheni mipango mbalimbali ya maendeleo na shida zake na namna ya
kukabiliana na shida hizo.
Katika
utafiti huo imeelezwa kuwa pamoja na uchumi wa Tanzania kukua kwa kasi
umaskini bado ni kero kubwa kutokana na kukosekana kwa uhusiano kati
ya ukuaji wa kiuchumi na kufutwa kwa umaskini miongoni mwa wananchi wa
kawaida. Kuanzia mwaka 2001 uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa zaidi ya asilimia 6.
Mratibu
huyo wa UN nchini amesema kwamba kutokana na kasi ya uchumi kutoenda
sambamba na uchumi ndio maana UN inashirikiana na serikali kuona namna
bora ya ukuaji uchumi kwenda sawa na uondoaji wa umaskini miongoni mwa
wananchi waliowengi.
Meza
kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa
Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo, Mgeni rasmi Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile na Mratibu Mkazi wa mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Wakati
huo huo serikali imesema imefurahishwa na uzinduzi wa ripoti hiyo
ambayo inatumaini itasaidia katika kuboresha sera na kujibu masuala
muhimu ya kukabiliana na umaskini nchini. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dk. Servacius Likwelile katika tukio hilo la uzinduzi wa ripoti.
Alisema
serikali inaamini kwamba mambo yaliyomo katika ripoti hiyo yatasaidia
katika harakati zake za kukabili umaskini ikiwa ni pamoja wa mipango ya
maendeleo kwa kuzingatia dira ya taifa ya maendeleo ifikapo mwaka 2025. Tanzania
inajipanga kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 ikitegemea
viwanda katika uchumi wake badala ya kilimo kama ilivyo sasa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi
kutoa hotuba ya uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Maendele0 ya Binadamu 2014
Tanzania uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Alisema
kwamba serikali imefurahishwa na jinsi ripoti ilivyojikita katika
kuainisha maendeleo ya watu na sehemu kubwa ya ushauri utazingatiwa kwa
mipango mipya ya maendeleo.
Ripoti
ya maendeleo ya watu ni mkakati wa serikali ya Tanzania ulianzishwa
Machi 2013 kwa lengo la kutafiti namna bora ya kunasua wananchi katika
umaskini wakati taifa likiendelea kukuza uchumi.
Mradi
huo unatekelezwa na taasisi ya ESRF ikishirikiana na Wakala wa taifa
wa Takwimu (NBS), Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa serikali ya Zanzibar na
kitivo cha uchumi cha chuo kikuu cha Dar es Salaam. Mradi
huo unafadhiliwa na UNDP na umejikita zaidi katika kuangalia
vipaumbele katika maendeleo, mambo yanayojitokeza, fursa na changamoto.
Mgeni
rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania,
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akitoa hotuba
kwenye uzinduzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni baadhi ya wadau waalikwa wakifuatilia htouba ya mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma risala
kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania
uliofanyika mwishoni mwa juma jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014, Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile akikata utepe kuzindua
rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania uliofanyika mwishoni
mwa juma jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia uzinduzi huo ni Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto)
na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii
(ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo (kulia).
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua
chapisho la Kiswahili la Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania
huku mgeni rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF wakishuhudia tukio hilo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo akizundua chapisho la kingereza la Ripoti ya Maendeleo
ya Binadamu 2014 Tanzania katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa juma.
Mgeni
rasmi kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania,
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwelile
(katikati), Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa
Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Hoseana Lunogelo kwa pamoja wakionyesha
ripoti hiyo kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa waliohudhuria
uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo (kulia), Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dk.
Servacius Likwelile (katikati) na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez wakipitia nakala za ripoti hiyo mara
baada ya kuzinduliwa rasmi jijini Dar.
Mgeni rasmi kwenye picha ya pamoja na wadau waliofanikisha maandalizi ya ripoti ya Maendeleo ya Binadamu 2014 Tanzania.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Hoseana Lunogelo (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi mkazi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Tanzania, Philippe Poinsot
(kushoto) wakati wa kupiga picha ya kumbukumbu. Kulia ni Mwakilishi
msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon
Manyama.
No comments:
Post a Comment