Na Mwandishi Wetu, Kilindi
MKUU wa Wilaya Kilindi, DC Selemani Liwowa,
amesema kwamba wilaya yake ipo katika hatua nzuri juu ya ukamilishaji wa suala
la ujenzi wa maabara, tangu walivyoanza mchakato huo mwaka jana.
Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Selemani Liwowa, pichani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi wilayani
Kilindi, DC Liwowa alisema kwamba shule nyingi zimeshakamilika kwa kiwango cha
asilimia 100, huku zile zilizosalia zikiwa katika hatua ya mwisho za (finishing),
jambo linalotia moyo.
Alisema kwamba akiwa kama DC wa Kilindi
alihakikisha kwamba agizo la Rais Jakaya Kikwete juu ya ujenzi wa maabara
linafanikiwa kwa vitendo, hivyo kuanza kulisimamia kwa nguvu zote kwa
kushirikiana na watendaji, watumishi na wananchi wote.
“Kidogo sisi tunaendelea vizuri na ujenzi wetu
wa maabara ambapo shule nyingi zimefikia hatua nzuri na nyingine zilizosalia
zimeshakamilika kwa asilimia zote kutokana na nguvu kazi na ushirikiano wa watu
wote katika wilaya yetu.
“Naamini kwa hatua hii ile dhana ya ujenzi wa
maabara itakuwa na mashiko kwa kuhakikisha kwamba shule za kata zilizosalia
ambazo ujenzi wake haujakamilika unafanyika nguvu na jitihada kubwa kukamilisha
mchakato huu muhimu,” alisema.
Licha ya mabadiliko kadhaa katika wilaya
mbalimbali kwa wakuu wake wa wilaya kuhamishwa, DC Liwowa ni kati ya wale
waliobakizwa kwenye vituo vyao vya kazi, jambo linalomfanya aendelee na program
zake alizokuwa akizifanya kwenye wilaya ya Kilindi.
No comments:
Post a Comment