Na Kambi Mbwana,
Aliyekuwa Handeni
AFISA Utamaduni
wilayani Handeni, mkoani Tanga, Godfray Munga, amesema kwamba kufanyika kwa
Tamasha la Utamaduni wilayani humo kumechangia kwa kiasi kikubwa kuitangaza
wilaya yao.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Tanga, Frank Maduga, akiperuzi katika gazeti huku akiwa ni miongoni mwa wadau waliohudhuria tamasha la Handeni Kwetu lililofanyika Jumamosi ya wiki iliyopita, wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Tamasha hilo lilifanyika Jumamosi
ya Desemba 14 mwaka huu, huku likishirikisha wadau mbalimbali sanjari na
viongozi wa serikali, ikiwamo ofisi ya Mkuu wa Wilaya Muhingo Rweyemamu.
Akizungumza mapema
wiki hii, Munga alisema akiwa kama Afisa
Utamaduni, amefurahi kuona eneo lake la kazi linakusanya watu wengi kwa ajili
ya kuenzi jitihada za maendeleo kwa kupitia sekta ya utamaduni.
“Hili ni jambo
ambalo limenifanya nione faraja sana
katika kuhakikisha kuwa utamaduni wa Mtanzania unaenziwa hususan kwa wakazi na
wananchi wa Handeni.
“Naamini mambo
yatazidi kuwa mazuri katika siku zijazo kulifanya tamasha lifike mbali zaidi
kwa kushirikisha wasanii na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,”
alisema.
Katika Tamasha hilo, mgeni rasmi alikuwa
DC Rweyemamu, ambapo alishuhudia umati wa watu ukihudhuria kwa mara ya kwanza
na kulifanya kwa mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment