YAH: MWALIKO WA
TAMASHA LA HANDENI 2013
Husika na kichwa cha habari hapo juu. Ukiwa kama mdau wa
Handeni, mwananchi na mzalendo wa Tanzania, unaombwa kuhudhuria Tamasha la
Utamaduni, maarufu kama ‘Handeni Kwetu 2013’, litakalofanyika katika Uwanja wa
Azimio, Jumamosi ya Desemba 14 mwaka
huu.
Katika tamasha hilo, tutapata fursa ya kuangalia ngoma
mbalimbali za utamaduni kutoka katika vijiji vya wilaya ya Handeni, kama vile
Kweingoma, Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni
Mjini.
Tunapenda sana kushirikiana na wewe katika tamasha hili
linaloanza kwa mara ya kwanza katika wilaya hii ya Handeni, mkoani Tanga.
Kuanzishwa kwa tamasha hili ni sehemu ya kushirikiana kwa karibu na viongozi wa
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika Tamasha hili, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa
Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Handeni, Dkt Abdallah Kigoda.
Tamasha hili litaanza na matembezi Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Handeni, saa
2:00 na kuelekea Uwanja wa Azimio, ambako huko litaisha saa 12 za jioni.
Kama mdau wetu wa maendeleo, tunakuomba tushirikiane kutangaza,
kuthamini na kukuza utamaduni wetu ili iwe njia ya kuchangia maendeleo yetu.
Hakuna kiingilio. Pia unaombwa kujigharamia mwenyewe katika ujio wako kwenye
tamasha hili. Tunashukuru kwa ushirikiano wako na unakaribishwa sana katika
Tamasha hili.
Wako katika Ujenzi wa Taifa.
Mratibu Mkuu
Kambi Mbwana
Contact: kambimbwana@yahoo.com
Wabsite: HANDENI KWETU, www.handenikwetu.blogspot.com
+255 712053949
+255 753806087
No comments:
Post a Comment