Na Mwandishi Wetu
Mabingwa wa muziki wa dansi nchini Msondo Ngoma na Mlimani
Park Orchestra “Sikinde” kesho mchana
zitachuana vikali katika viwanja vya TCC Club
Chang’ombe, Temeke.
Mpambano huo wa kusherekea sikukuu ya Krismasi litakuwa la kufunga
mwaka 2013 na pia litaamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wa muziki wa
dansi nchini mwaka huu.
Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano huo
litanzaza saa nane alasiri hadi majogoo.
Vijana wa Msondo Ngoma pichani.
Kapinga alisema Sikinde wataingia TCC wakitokea Bagamoyo
walipokuwa wakipiga kambi wakati kambi ya Msondo Ngoma imebaki kuwa siri kwa
muda wote.
Mratibu huyo alisema kila bendi litapiga kwenye jukwaa lake ili
kuondoa hujuma.
Kapinga alisema kila bendi itatapewa muda wa saa moja kupiga
jukwaani kabla ya kumpisha nyingine.
Kiongozi wa Msondo Ngoma Saidi Mabera
alisema jana kuwa watapiga nyimbo zao zote kali ili kuhakikisha
wanaibuka kidedea.
Alitaja
baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni
'Nimuokoe Nani', 'Zarina', 'Mwanaidi', 'Kanjelenjele', 'Bahati',
'Sesilia', 'Usiue Usiibe', 'Asha Mwana Seif', 'Kauka Nikuvae', Chuma Chikoli
Moto', 'Kilio cha Mzima', 'Ajali' na
'Suluhu'.
Baadhi
ya wanamuziki wanaounda Msondo Ngoma ni Shaaban Dede, Mabera, Abdul Ridhiwani
Pangamawe, Athumani Kambi, Saad Ally 'Mashine', Eddo Sanga, Huruka Uvuruge,
Zahoro Bangwe, Ibrahim Kandaya, James
Mawilla, Juma Katundu, Hamisi Mnyupe,
Roman Mng’ande `Romario’ na Hassan
Moshi.
Naye kiongozi wa
Sikinde Hamisi Mirambo alijigamba kuwa wataibuka na ushindi mnono.
“Tuna
waimbaji wazuri na hakuna itakachotuzuia kushinda,” alisema Mirambo.
Alitaja
baadhi ya nyimbo ambazo watazipiga kuwa ni
'Selina', Wiki
endi', 'Penzi la Fukara', 'Hiba', 'MV Mapenzi’,
'Supu Umelitia Nazi' na 'Jinamizi la Talaka'.
Sikinde inaundwa
na wanamuziki kama Hassan Rehani Bitchuka, Hassan Kunyata, Kaingilila Maufi,
Tonny Karama, Shaaban Mabuyu, Habib Abassi, Juma Choka, Ally Jamwaka, Mbaraka Othman, Hamisi Milambo, Shaaban
Lendi, Joseph Benard, Ramadhani Mapesa na Habibu Jeff.
Pambano umeandaliwa
na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi, Nipashe, CXC
Africa na Saluti5.
No comments:
Post a Comment