Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
UJIO
wa mwanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu, Catherine Cindy umeleta kicheko kwa
viongozi wake, baada ya kuwa nje ya nchi kwa miezi mitatu.
Meneja wa Mapacha Watatu, Hamis Dacota, katikati akiwa na wanamuziki wake, Jose Mara kulia na Khalid Chokoraa kushoto.
Cindy
aliwasili nchini juzi akitokea nchini Japan,
hivyo kusubiriwa kwa hamu na wadau wa bendi hiyo inayoongozwa na Khalid
Chokoraa na mwenzake Jose Mara kama
wakurugenzi.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam,
Meneja wa Mapacha Watatu, Khamis Dacota, alisema kuwa mwanadada huyo ameleta
uhai zaidi kutokana na ubora wake jukwaani.
“Catherine
si mtu wa kawaida na kila mdau wa muziki wa dansi anafahamu uwezo wake, hivyo
sisi wote tumefarijika na kurejea kwake,” alisema.
Mwanadada
huyo ni miongoni mwa vijana wadogo wenye ujuzi wa kucheza na sauti zao, huku
makali yake yakitarajiwa kumuweka juu mno katika tasnia ya muziki wa dansi hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment