Na Kambi
Mbwana, Handeni
NI jambo la
kawaida mchezaji yoyote kuandikwa katika vyombo vya habari, hususan magazeti,
ukaona kesho anasajiliwa na klabu ya Simba, tena bila hata kuridhishwa na
kiwango chake ndani ya benchi la ufundi.
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage
Ukitaka kulizungumzia jambo hili, utaona jinsi gani viongozi wa klabu za soka Tanzania, hasa za Simba na Yanga wanapoingia katika majaribu ya kuchukua mchezaji ili mradi ameng’aa kihabari.
Ukitaka kulizungumzia jambo hili, utaona jinsi gani viongozi wa klabu za soka Tanzania, hasa za Simba na Yanga wanapoingia katika majaribu ya kuchukua mchezaji ili mradi ameng’aa kihabari.
Wakati
mwingine mchezaji huyo amewekwa gazetini si kwa sababu ana kiwango kizuri, hivyo
endapo viongozi wa soka wataendelea na mpango wao wa kusajili kwa kuangalia
gazeti limeandika nini, hakika hatuwezi kuendelea.
Hapa ndipo
nisipoweza kuvumilia. Hatuwezi kuendelea, kama vyombo vya habari ndivyo vitakavyosajili.
Hii ni kwasababu, mara kadhaa mchezaji anayeandikwa kupita kiasi, si kama ana
kiwango cha juu.
Na kiwango
hicho inastahili kuonekana mbele ya kocha wa timu husika na kwa viongozi
wanaotumika kusajili, wakiamini wataonekana ni wachapakazi mbele ya wanachama
na wadau wa soka.
Ukiangalia
kwa sasa, vyombo vimegeukia kwa kipa Yaw Berko. Huyu aliwahi kucheza ndani ya
Yanga kabla ya kuondoka akidaiwa kuwa kiwango chake kimeshuka.
Berko sasa
anapigiwa chapuo na wadau akihusishwa na mipango yake ya kujiunga na Simba,
timu pinzani na ile aliyoichezea hapa Tanzania.
Jumamosi
iliyopita, Berko alitarajiwa kuwasili nchini, tayari kuingia makubaliano na
Simba, katika michuano ijayo, ikiwamo Ligi ya Tanzania Bara, mzunguuko wa pili,
utakaoanza Januari mwakani.
Inashangaza
kama viongozi wetu wa soka watakuwa wakisajili kwenye magazeti, jambo ambalo
haliwezi kuendeleza soka la Tanzania. Tunahitaji viwango vilivyothibitishwa na
makocha wetu.
Wao ndio
wanaofahamu wapi kwenye mapengo kwa ajili ya kuboresha vikosi vyao, hivyo kuna
kila sababu ya kubadilisha nyendo zetu kama kweli tunahitaji kusonga mbele.
Huo ndio
ukweli wa mambo. Lakini kusajili wale walionekana kwenye magazeti wakati
mwingine si dawa ya kukuza soka, isipokuwa njia mbaya ya kulidumaza soka letu
linalokwenda mbele na kurudi nyuma.
Hakika
siwezi kuvumilia. Siwezi kuvumilia hii haitokani na mtazamo wa kumsajili Berko,
ila ni pale tutakapoendeleza maisha ya kusajili kwa kupitia vyombo vya habari,
tena bila kuangalia mahitaji ya benchi la ufundi.
Tukifanyaa
hivyo, miaka nenda rudi Tanzania itaendelea kuwa kichwa cha mwendawazimu maana
si kila mmoja ana bahati ya kuandikwa katika vyomb hivyo, jambo linaloweza
kuwafifisha wale wenye uwezo wa juu wa kucheza soka na wanaopata nafasi wakiwa
wale wa kawaida.
Tukutane
tena wiki ijayo.
+255
712053949
No comments:
Post a Comment