Msimamizi wa Mchezo wa ngumi katika kambi iliyopo sinza
makaburini,
Bernald Lumbila (kushoto) akimwelekezai bondia Kalama Nyilawila jinsi
ya kupiga ngumi katika mbavu Dar es saam Nyilawila anajiandaa na
mpambano wake dhidi ya Ibrahimu Maokola utakaofanyika Desemba 31 katika Ukumbi wa Msasani Clabu.
Kalama Nyilawila akijifua
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BONDIA Kalama Nyilawila yupo katika
mazoezi makali ya mwisho mwisho kabla ajamkabili mpinzani wake Ibrahimu
Maokola siku ya Desemba 31 mpambano wa kufunga mwaka utakaoshirikisha
mabondia mbalimbali akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kalama
ameseme yeye yupo fiti wakati wowote kwa ajili ya mpambano huo kwa ana
usongo wa kuonesha ngumi zinachezwaje kwa mabondia chipkizi nchini
Mpambano huo utaanza kabla ya bondia
Fransic Miyeyusho kupanda jukwaani kuvaana na David Chalanga kutoka
Kenya mpambano wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi.
Na mapambano mengine ni Ibrahimu Class
'King Class Mawe' atavaana na Mohamed Kashinde uku Cosmas Cheka
akioneshana ubabe na Iddy Mnyeke mpambano mwingine ni Antoni Mathias
atakae menyana na Fadhili Majiha mapambano yote ya utangulizi ni ya
raundi sita sita
siku hiyo itasindikizwa na burudani za
kila aina akiwemo mwana hi pop mashuhulu Kala Pina, Kimbunga Noma na
wengine wengi ambao wata uanga mwaka na kukaribisha mwaka mpya kwa njia
ya burudani.
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa
na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria
zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Manny Paquaio, Saul 'canelo' alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia
kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikitolewa na Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa pesa
taslimu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha
No comments:
Post a Comment