https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Sunday, December 29, 2013

Handeni wazitamani Simba na Yanga kukipiga kwenye Uwanja wa Azimio wilayani kwao


Na Kambi Mbwana, Aliyekuwa Handeni

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, mkoani Tanga, Thomas Mzinga, amesema kwamba Uwanja wao wa Azimio unastahili kukutanisha vigogo vya Simba na Yanga, katika michuano yoyote nchini.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni, Thomas Mzinga, pichani.
Akizungumza na Handen Kwetu Blog mapema wiki hii wilayani Handeni, Mzinga alisema kuwa hiyo ni kutokana na maandalizi na mwonekano wa uwanja wao wa michezo.


Alisema kuwa Uwanja wao ni mkubwa na unastahili kukutanisha timu kubwa na vigogo wa Tanzania Bara, vikiwapo Simba na Yanga.


“Tunajivunia kuwa na uwanja mzuri na muwajulishe huko kuwa wanapaswa waje wacheze huku katika mashindano yao mbalimbali.


“Tunaamini Uwanja huu pia ukikamilika kwa baadhi ya ukarabati wake, basi utachangia kwa kiasi kikubwa kuleta watu mbalimbali, hasa timu kubwa zitakapokuja,” alisema Mzinga.


Hata hivyo, kiu ya Mzinga na viongozi wa serikali wilayani humo inaweza kutimia kama wataipigania au kuwashawishi viongozi wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuhakikisha kuwa timu ya JKT Mgambo itaufanya Azimio kuwa uwanja wake wa nyumbani.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...