Ujumbe wa Mjasiriliamali
Mwishoni mwa mwezi
Februari mwaka huu; nilijichimbia wilayani Mvomero-Morogoro kujifunza na
kuangalia fursa ya uanzishaji na uendelezaji wa mashamba ya mifugo
(lanchi). Baada ya kumaliza kilichonipeleka, nikiwa na rafiki yangu
mjasiriamali anaepambana kwa spidi ya ajabu; George Kisawani,
tulipata wasaa wa kumtembelea mama mmoja aitwaye Veronica Urio mkulima
aliyefanikiwa sana katika kilimo cha mpunga, anaeishi maeneo ya Dakawa.
Albert Nyaluke Sanga kulia, akiwa na mjasiriamali Veronika Urio.
Mama
huyu alinigusa mno, kwani amekuwa ni mkulima namba moja aliyepewa tuzo
ya US AID kupitia mradi wa Feed the Future; kutokana na kufanikiwa
kulima kilimo cha kisasa . Kwa mafanikio yake alilikuna hadi baraza la
senete la Marekani kiasi ambacho mwaka 2011, walitumwa maseneta wawili
kuja katika mashamba ya mama huyu kushuhudia na kujifunza namna
anavyofanikiwa katika kilimo hiki cha mpunga ambapo huvuna maelfu ya
magunia kila msimu. Kwa kilimo hiki mama huyu anamiliki vitega uchumi
vingi kiasi kwamba amepata uthubutu wa kusomesha watoto wake watatu
katika nchi za Marekani, Ujerumani na Poland.
Kilichonikosha ni kuwa
mama huyu kielimu ni darasa la saba tu lakini amekuwa ni mtu anaependa
kujifunza, kudadisi na kutafuta taarifa sana. Kutokana na faida
anayovuna kutoka katika kilimo hicho, amejiwekea utaratibu wa kufanya
safari za mapumziko katika nchi za Ulaya na Asia kila mwisho wa msimu wa
kilimo. Katika mazungumzo yetu mama huyu alitueleza hivi:
"Nina jumba
la kifahari na kitanda kizuri sana, lakini sikumbatii kitanda
kupitiliza. Kila siku ninaamka saa kumi na moja alfajiri na ninarudi
nyumbani usiku. Kila mara popote nilipo ninaumiza kichwa ni namna gani
nitaendelea kuongeza uzalishaji" Mwisho akatupa wosia,
"Ikiwa mimi mama
yenu na umri huu bado ninajituma kupambana, je, ninyi vijana kwa nini
mzembee wakati mna nguvu na uwezo kunishinda? Kuweni ngangari, msilale,
changamkeni kuandaa maisha mkingali vijana kwa sababu fursa za kuwa
mabilionea zipo katika FIKRA ZENU" ~SmartMind~
No comments:
Post a Comment