Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MWENYEKITI wa Kamati ya Gurumo (55) Asha Baraka, amembana
mratibu wa tamasha hilo
Juma Mbizo kwa kumtaka ampelekee ripoti ya matukio yalivyoandaliwa na kufanyika
katika onyesho la kumuaga Muhdin Gurumo, lililofanyika Jumamosi ya Desemba 14
mwaka huu.
Mwenyekiti wa iliyokuwa Kamati ya Gurumo, Asha Baraka kulia, katika matukio ya kufanikisha tamasha la mzee Gurumo.
Asha aliyasema hayo huku kukiwa na habari mbaya kutoka kwa baadhi ya wadau waliolalamikia maandalizi pamoja na mgawo wa fedha kwa wale walioalikwa, ukiachwa walioamua kujitolea.
Asha aliyasema hayo huku kukiwa na habari mbaya kutoka kwa baadhi ya wadau waliolalamikia maandalizi pamoja na mgawo wa fedha kwa wale walioalikwa, ukiachwa walioamua kujitolea.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam,
Asha alisema kwamba wakati tamasha hilo la
kumuaga Gurumo linafanyika alikuwa nje ya nchi, hivyo amemtaka Mbizo kama mratibu apelike ripoti.
Alisema mara baada ya kuipata ripoti hiyo, kila kitu
kitakuwa wazi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu sawa na kulinda heshima kwa wadau
wa muziki, wakiwamo wale wanaolalamikia mchakato huo.
Kwa sasa siwezi kusema lolote kwasababu sijapata ripoti
ingawa tayari nimeshazungumza na mratibu, Juma Mbizo nikimuomba ailete kwa
ajili ya kuangalia jinsi shoo ilivyofanyika,” alisema Asha.
Tamasha hilo liliandaliwa kwa
ushirikiano mkubwa wa wadau wa muziki, akiwamo Asha kama
mwenyekiti, Said Mdoe, Mbizo na wengineo kwa ajili ya kumuaga Gurumo kutokana
na kuachana na muziki.
No comments:
Post a Comment