Na Kambi Mbwana, Dar
es Salaam
MWENYEKITI wa Tawi la Mpira Pesam Ustadh Masoud, amesema
moto wa kutokuwa na imani na mwenyekiti wao Ismail Aden Rage umesambaa nchi
nzima, kutokana na kiburi anachoonyesha mwenyekiti wao.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita, Masoud alisema
kwamba Rage ni mbishi asiyependa kusikiliza ushauri wa mtu yoyote, huku
akijidanganya kwamba ni Mpira Pesa tu wasiyokuwa na imani naye.
Alisema mara kadhaa Rage anatushutumu sisi Mpira Pesa, ila
wakati huu kila mtu anayeipenda Simba hafurahishwi na mwenendo wa mwenyekiti
wetu, ndio maana hata ushauri aliyopewa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ya
kuitisha Mkutano ameshindwa kuutekeleza.
“Sio Mpira Pesa tu wanayeumizwa na mwenendo wa mwenyekiti
wetu Rage, maana nchi nzima sumu yake imezagaa, hivyo nadhani ni wakati wake
kukaa na kusikiliza malalamiko ya wanachama wake,” alisema.
Sakata la mgogoro wa Rage ndani ya klabu ya Simba unazidi
kushika kasi, jambo ambalo lilisababisha TFF wao wamtake aitishe mkutano kwa
ajili ya kumaliza tofauti zake na wanachama wake, ingawa ushauri huo
haujafanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment