Baadhi
ya wananchi kutoka katika vijiji mbalimbali vya Wilaya ya Handeni
wakiandamana kuelekea katika viwanja vya Azimio, kuhudhuria msimu wa
Kwanza wa Tamasha la Utamaduni Handeni Kwetu 2013, Tumethubutu na
kufanikiwa tunasonga mbele...
Akizungumza wakati wa
kutambulisha wadhamini na wahisani mbalimbali waliofanikisha kufanyika
kwa Tamasha hilo, mratibu wa Tamasha la utamaduni Handeni 2013, Kambi
Mbwana alisema udhamini wa NSSF ulikuwa mkombozi mkubwa
kwao.
“Awali ya yote napenda kutanguliza shukrani zangu zote kwa wahisani
wa
tamasha hili, hasa ndugu zetu wa NSSF maana hakika wameonyesha moyo wa
uungwana katika kuhakikisha kuwa Handeni Kwetu inazaliwa kwa mafanikio,
ukizingatia kuwa tamasha hili limekusanya watu wa aina mbalimbali.
Awali
akizungumza baada ya kuzindua Tamasha hilo ambalo lengo lake lilikuwa
ni kuwakutanisha watu wa Handeni kusherekea utamaduni wao pamoja na
kukumbusha umuhimu wa kujenga Handeni, Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya
Handeni, Muhingo Rweyemamu, alisema kwa kuwa na Matamasha kama hayo
jamii inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kupata Maendeleo wanayoyataka.
Muhingo
alisema ili mafanikio yapatikane katika kila jambo ni lazima watu wa
eneo fulani wawe na utayari wa kukutana na kujadili mambo yao kwa sauti
kama waratibu wa tamasha hilo walivyofanya.
“Tunajivunia kuwa na
vijana wenye mawazo mapana kama haya, naambiwa tamasha hili ni matokeo
ya mawazo ya kimaendeleo ya vijana wetu, hongereni sana,” alisema
Rweyemamu.
Kwa upande wake, Meneja wa NSSF, mkoani Tanga, Frank
Maduga alisema shirika hilo limedhamiria kuendelea kushirikiana na
waaandaaji wa tamasha hilo kwa lengo la kuhakikisha Utamaduni wa
Mtanzania unatumika kulitangaza Taifa, pamoja na kutumia fursa hiyo
kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa kutoa elimu ya huduma zao wilayani
Handeni na Tanzania kwa ujumla.
"NSSF ni shirika la Watanzania
na tumedhamiria kuwapatia huduma bora Watanzania wote, hivyo kila mtu
ana haki ya kujiunga na mfuko huu kwa ajili ya kujiwekea mazingira
mazuri katika wakati wote wa maisha yake," alisema Maduga.
Katika
tamasha hilo,kulikuwa na vionjo mbalimbali vya Utamaduni wa
Wanahandeni, ikiwa ni Pamoja na Ngoma za
asili kutoka katika Vijiji vya wilaya ya Handeni kama vile, Kweingoma,
Kwamatukutu, Kwediamba, Kwachaga pamoja na vikundi vingine vya Handeni
Mjini.
Burudani kali na ya kuvutia iliyoonesha asili kamili ya
Mtanzania ilitoka kwa Kundi la Sanaa la Jeshi la JKT Mgambo, Azimio Jazz
band bila kusahau msanii wa kundi la Fataki, Machenja ambaye alipiga
onesho la kukata kiu akiwa na wana okalandima.
Tamasha la
Utamaduni Handeni ambalo linafanyika kwa mara ya Kwanza lilidhaminiwa na
NSSF, Clouds FM, Vodacom, Plan B, gazeti la Mwananchi, Kajunason Blog,
Chichi Local Wear, Katomu Solar specialist, Dullah Tiles and Construction, Anesa Company Limited, Country Business directory, Jiachie Blog na Taifa Letu.com. |
No comments:
Post a Comment