Na
Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MSANII
chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Ahmad Salum ama (Mady Salu), amesema
kwamba ili aweze kushiriki katika Tamasha la Handeni Kwetu ilimlazimu aingie
Studio kurekodi wimbo uliokwenda kwa jina la ‘Safari ya Tanga’.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam,
Mady Salu alisema kwamba hatua hiyo ilisababishwa na uchu wake wa kupania
kupanda katika jukwaa la tamasha lililofanyika kwa mara kwanza.
Alisema
mara nyingi wasanii wachanga wamekuwa wakipata nafasi hiyo mara chache mno,
hivyo nafasi yake ya kupangwa kuwapo katika tamasha hilo kulimfanya ajiandaye vizuri.
“Nisingepata
nafasi ya kushiriki ningeumia kwakuwa niliambiwa namna gain ya kufanya ili
niweze kufanya vyema katika tamasha.
“Tamasha
lilihusu utamaduni, hivyo kitendo cha kurekodi wimbo wangu wa Safari ya Tanga
hakika ulinitangaza vizuri na kuonyesha pia shauku ya kutangaza kipaji changu
katika muziki wa kizazi kipya,” alisema.
Mady
Salu aliwahi kuwapo katika kundi la Ngovita Clew lililotambulisha wimbo wa
Maisha Miangaiko, ambalo baadaye liligawanyika.
No comments:
Post a Comment