Allan Kalinga-CEO for Afro-Euro Management Co. LTD
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAIMBAJI kutoka nchi tano katika Kanda ya Afrika Mashariki hadi kufikia
mwisho wa mwaka huu wanatarajiwa kushiriki katika shindano jipya la
uimbaji liitwalo Shindano la Waimbaji wa Afrika Mashariki.
Shindano
hilo ambalo limeandaliwa na Kampuni ya Afro-Euro Events Management Co.
Limited, linatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam, na kuhusisha
wasanii nguli kutoka Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda na Burundi.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Afro-Euro Management Co. LTD,
Allan Kalinga, ambaye kwa sasa makazi yake yako nchini Uingereza,
alisema kwamba wagombea husika watachuana kuwania tuzo ya heshina ya
juu kuvikwa taji la muimbaji bora wa eneo la Afrika Mashariki.
"Umma wa Afrika Mashariki utahusishwa kuanzia mwanzo wa shindano
hili hadi mwisho na hivyo mshindi atakayepatikana atakuwa chaguo la
kweli la watu wa Afrika Mashariki, " alisema Kalinga.
MCHAKATO WA UTEUZI
Kalinga aliendelea kusema zaidi kwamba kila nchi shiriki itafanya
uteuzi wake wenyewe kuwatambua wanamuziki wake watano bora ambao
watawakilisha katika fainali ya kikanda.
"Kila nchi itakaribisha
raia wake kutuma mapendekezo yao kuhusu mwanamuziki bora kwa kutumia
namba ya Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) kupitia shirika la simu
litakaloteuliwa kwa kipindi cha muda maalum . Shirika hilo la simu
litakaloteuliwa litaingia makubaliano na kampuni ya Afro-Euro Management
Co. LTD kuhusu gharama za ujumbe mfupi wa maneno (SMS) na mpangilio wa
kugawana mapato, "alibainisha.
Majina yaliyopendekezwa yatalingana na wanamuziki watakaoshika
nafasi za juu nne watakuwa wawakilishi wa nchi husika katika shindano ka
kikanda.
Kwa mujibu wa Kalinga, idadi ya mwisho kwa washiriki kutoka
nchi hizo tano itakuwa 25 na hawa ndio wanamuziki watakaoshindana
katika Shindano la Waimbaji wa Afrika Mashariki Dar es Salaam.
MUUNDO WA SHINDANO
Amebainisha kwamba washiriki 25 waliofuzu
fainali watagawanywa katika makundi manne ya waimbaji watano, na kila
mwimbaji katika kundi atatakiwa kutoka kutoka nchi tofauti.
"Kundi
la kwanza lifanya onesho Jumamosi ya kwanza baada ya kutangazwa
wateule 25 watakaoshiriki fainali. Watawasili nchini siku ya Ijumaa, na
kufanya onesho Jumamosi na kuondoka Jumapili. Maonesho yatakuwa juu ya
jukwaa na kuoneshwa moja kwa moja kwa njia ya televisheni katika nchi
zote tano za Afrika Mashariki na vituo vya Televisheni
vitakavyoteuliwa, " alisema Kalinga.
Baada ya maonesho na kwa siku ya sita zitakazofuata, anasema kwamba
umma utaalikwa kupiga kura kupitia SMS kwa kutumia namba maalum katika
mitandao itakayoteuliwa kwa ajili ya kuwateua wasanii wao bora kati ya
kikundi.
"Kura za kundi la kwanza zitajumlishwa na kuthibitishwa na kampuni
huru ya ukaguzi wa hesabu, na kutangazwa wakati wa maonesho ya kundi la
pili siku ya Jumamosi. Waimbaji watakaoshika nafasi mbili za juu kutoka
kila kundi watafuzu fainali, na hivyo kutupa jumla ya waimbaji 8
watakaoshiriki fainali, " alibainisha.
Katika kila wiki wakati kura zikiendelea, vyombo vya habari ambavyo
kampuni ya Afro-Euro Management Co. LTD itashirikiana navyo katika
kila nchi zitangaza upigaji kura kwa njia ya 'SMS' katika nchi husika
za Afrika Mashariki ya Afrika ili kupata watu wengi iwezekanavyo
kushiriki.
Aidha, Kalinga, ambaye pia kampuni yake ya Afro-Euro Management Co.
LTD ndiyo iliyoratibu shindano la ulimbwende la Miss Afrika in UK
lililofanyika katika jiji la Reading nchini Uingereza mwaka 2004 -
alisema washiriki nane wa fainali kisha watashindana katika Finali Kubwa
(Grand Finale).
FAINALI KUBWA
"Jumamosi ya wiki ya tano, washindi wa kundi la
mwisho wataungana na washiriki wengine sita waliofuzu fainali katika
kufanya maonyesho yao katika Fainali Kubwa . Umma kutoka nchi shiriki
kisha utakuwa na siku sita (Jumapili hadi Ijumaa) za kupiga kura
kumchagua mshindi pekee, " Kalinga alisema.
Alibainisha kwamba matokeo yatajumuishwa baada ya upigaji kura
kufungwa Ijumaa ya wiki ya sita na kuthibitishwa na kampuni huru ya
ukaguzi wa hesabu kabla ya tangazo la mwisho la matokeo Jumamosi wakati
wa onesho la mwisho litakalooneshwa moja kwa moja kwa njia ya
televisheni, akiongeza kuwa idadi ya kura zilizopigwa kwa kila aliyefuzu
fainali itaamua ni nani itatangazwa mshindi, mshindi wa pili na mshindi
wa tatu.
TUZO & ADA
Aliongeza kusema kwamba kampuni yake ataamua
zawadi kwa mshindi, mshindi wa pili na mshindi wa tatu; Na uimbaji/ada
ya uimbani kwa washiriki 25 waliofuzu fainali.
MIPANGO YA BAADAYE
Mkurugenzi
Mtendaji huyo alibainisha kwamba sehemu ya faida kutokana na shindano
hilo itakwenda kwa taasisi ya hisani itakayochaguliwa katika kila nchi
shiriki.
Katika siku zijazo, inatazamiwa kwamba raundi ya mtoano katika
makundi manne itafanyika katika nchi shiriki nne tofauti huku Fainali
Kubwa ikifanyika katika nchi ya tano.
"Tunapanga kuingiza
shindano la pili, yaani Shindano la Waimbaki wa Injili Afrika Mashariki.
Tunaona mashindano hili litaendana na Shindano la Waimbaji wa Afrika,
ambapo bara la Afrika litagawanywa katika kanda, Afrika Magharibi,
Afrika Mashariki, Afrika Kaskazini, Afrika ya Kati na Kusini mwa Afrika,
"alisema.
Kuweza kumudu changamoto hii kubwa katika kuandaa na kuendesha
mashindano hayo ya kikanda, Kampuni ya Afro-Euro Management Co. LTD,.
Inakusudia kuteua kampuni za wakala kushikilia haki za mashindano katika
kanda zao husika.
Washindi na washindi wa pili wa kila kanda ya mashindano watafuzu
Fainali Kubwa (Grand Finale) ya Shindano la Waimbaji wa Afrika.
ONESHO LA MOJA KWA MOJA
Aidha,
Kalinga amesema kwamba washiriki 10 waliofuzu fainali watachuana katika
tamasha litakalooneshwa moja kwa moja katika televisheni litakaloitwa
TAMASHA LA AFRIKA MASHARIKI.
"Wasanii kumi kutoka nchi tano za Afrika Mashariki watafanya
maonesho katika majiji matano katika wiki tano mfululizo ili kuwapa
mashabiki wa muziki fursa ya kuona maonesho ya muziki moja kwa moja
kutoka kwa wasanii wakubwa katika Afrika ya Mashariki, "alisema.
No comments:
Post a Comment