https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, July 11, 2014

Japan wasaidia Dola Milioni 1.4 kwa ajili ya wakimbizi

DSC_0056
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (katikati) mara baaada ya kuwasili kwenye hafla fupi ya kukabidhi msaada wa dola za kimarekani milioni 1.4, kwa shirika la Chakula duniani (WFP) kwa ajili ya kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma. Kulia ni Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada.

Na Mwandishi wetu
Serikali ya Japan imetoa msaada wa dola za kimarekani milioni 1.4, kwa shirika la Chakula duniani ili liweze kuwasaidia wakimbizi zaidi ya 70,000 wakiwemo watoto 14,000 wanaohitaji Chakula katika kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
Akikabidhi msaada huo, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, aliwashukuru wafanyakazi wa shirika la Chakula duniani wanaofanya kazi Tanzania kwa kusaidia hali ya maisha ya Wakimbizi katika kambi zao.
Akizungumza katika halfa hiyo, Okada alisema nchi jirani na Tanzania zimekuwa katika vita zilizosababisha machafuko, lakini Tanzania kwa upande wake imekuwa ikiwapokea kwa wema Wakimbizi hao hivyo inapaswa kuungwa mkono kusaidia tatizo hilo la Wakimbizi
Balozi Okada alikabidhi pia tani 91 za mafuta ya kupikia, tani 367 za Unga wa nafaka, tani 400 za Maharage na tani 444 za Mahindi.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani hapa nchini Richard Ragan aliishukuru serikali ya Japan kwani imekuwa ikisaidia Wakimbizi kwa miaka mitano iliyopita.
DSC_0069
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe (katikati) akibadilishana mawazo mara baada ya kuwasili kwenye Bandari ya Dar na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan (kulia) pamoja na Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada.

Alifafanua kuwa msaada huo utasadia watu 70,000, wakiwemo watoto chini ya umri wa miaka mitano ambao idadi yao inakadiriwa kufikia 14,000 na akina mama wajawazito wanaokadiriwa kufikia 3,150.
Alisema kuwa pesa hizo zitasaidia pia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwani Maharage zaidi ya tani 400 yatanunuliwa humu nchini. Alibainisha kwamba kwa mwaka uliopita shirika hilo limetumia zaidi ya dola milioni 10 za kimarekani kununua chakula kwa ajili ya wakimbizi hapa nchini.
DSC_0078
Mshereheshaji wa hafla hiyo Afisa Habari wa WFP, Fizza Moloo akiwakaribisha wageni waalikwa kwenye halfa hiyo iliyofanyika jana jijini Dar kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mathias Chikawe aliwashukuru wafadhili wote ambao wamekuwa wakisaidia wakimbizi kwa miaka mingi.
“ninawashukuru wote kwa pamoja kwa misaada yenu kwa kusaidia tatizo la wakimbizi nchini kwetu kwa roho moja jambo linalomaanisha tunasaidiana katika kuubeba huu mzigo” alisema Chikawe.
Hata hivyo Chikawe alisema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jumuiya za kimataifa imekuwa ikitoa misaada ya kuwarejesha Wakimbizi makwao hali ya vita ikitulia na kwa kipindi cha zaidia ya miaka kumi serikali imewarejesha wakimbizi zaidia ya laki sita.
Aliahidi kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kutafuta suluhisho la kusaidia Wakimbizi, huku akiwahakikishia wafadhili kuwa milango ipo wazi waendelee kutoa ushirikiano kwa mujibu wa tamko la Geneva la mwaka 1951.
DSC_0170
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akisoma hotuba yake kwenye sherehe fupi ya kukabidhiwa msaada wa Chakula kwa ajili ya kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma uliotolewa na Serikali ya Japan.
DSC_0109
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akisoma risala wakati sherehe fupi za kukabidhi msaada wa Chakula kwa Serikali ya Tanzania zilizofanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam jana.
DSC_0083
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati hafla fupi ya makabidhiano ya Chakula cha msaada kilichotolewa na Serikali ya Jaapa kupitia Balozi wake hapa nchini.
DSC_0185
Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada akikabidhi msaada huo kwa Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan (kulia) kwenye hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar.
DSC_0178
Kaimu Meneja wa Bandari Bw. Nelson Mlali (kulia), Kaimu Afisa Mkuu wa Mawasiliano Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Peter Millanzi 9katikati) na Bw. David Mbonika wa WFP (kushoto) wakishuhudia tukio hilo.
DSC_0143
DSC_0147
Sehemu ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Bandari waliohudhuria halfa hiyo.
DSC_0193
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Mathias Chikawe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo kwenye hafla fupi iliyofanyika jana jijini Dar. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Mh. Masaki Okada na Kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan.
DSC_0010
Afisa Uhusiano na Siasa Ubalozi wa Ujerumani, Bw. Benedict Kikove (katikati) akijadiliana jambo na Afisa Habari wa WFP nchini, Bi.Seetashma THAPA (kulia) na Mtafiti na Mshauri wa masuala ya uchumi wa Ubalozi wa Japan nchini, Bi. Tamaki Yoshida mara baada ya tukio hilo.
DSC_0019
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani nchini (WFP), Bw. Richard Ragan (kushoto) akifurahi jambo na Bw. David Mbonika wa WFP (kulia) pamoja na Brian Mahemba wa African Marine Surveyors and Consultant Ltd. (katikati) mara baada tukio hilo.
DSC_0214
Baadhi ya wafanyakazi wa Bandari wakiandaa msaada huo tayari kupakiwa kwenye gari kupelekwa kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma.
DSC_0243
Forklift ikiingiza sehemu ya msaada huo kwenye Lori maalum lililoandaliwa kusafirisha mzigo huo.
DSC_0009
Pichani juu ni sehemu ya msaada huo uliokabidhiwa jana jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyofanyika Bandari ya Dar.
DSC_0004

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...