https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Tuesday, July 08, 2014

Benki ya Twiga Bancorp yaendelea kufanya mambo Viwanja vya Sabasaba

 Wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp wakiwa katika picha ya pamoja nje ya banda lao mapema leo, kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam.

 Mama Mjasiliamali wa kampuni ya Tree of Life,Bi.Jessica Msamba akifafanua jambo kwa  Afisa Masoko wa Twiga Bancorp,Bwa.Adalbert Alchard mapema leo mchana kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam.Bi Jesca ni mmoja wa wateja wakubwa wa benki hiyo na amekuwa akiendesha biashara zake za ujasiliamali kupitia mikopo mblimbali ya benki ya  Twiga Bancorp.
 Mkuu wa Shughuli za Kibenki wa Twiga Bancorp,Bwa.Richard Kombole akielezea jambo kwa baadhi ya Wanahabari hawapo pichani,mapema leo kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam,waliotaka kufahamu huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo kwa wateja wao,kulia ni Meneja wa Tawi wa benki hiyo Makao Makuu jijini Dar,Bwa.Sigisbert  Komba na nyuma ni Msimamizi wa Usalama wa Majengo benki ya Twiga Bancorp.
 Afisa Masoko wa Twiga Bancorp, Bwa.Adalbert Alchard akihojiwa na moja ya chombo cha habari,mapema leo mchana kwenye  maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa jijini  Dar es Salaam, kuhusiana na huduma wazitoaza kwa wateja wao, Bwa.Adalbert amesema kuwa benki yao,Twiga Bancorp inatoa huduma mbalimbali kama vile Akaunti ya Akiba,Akaunti ya Biashara,Akaunti ya Amana,Huduma za Kibenki za Kimataifa,mikopo,utumiaji wa fedha na nje ya nchi,''Dira yetu kubwa ni kuwa taasisi ya kifedha inayoongoza kutoa huduma bora za kibenki nchini'',alisema Bwa.Adalbert.
 Baadhi ya Wateja walipatiwa vipeperushi vilivyosheheni huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo ya Twiga Bancorp.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...