https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, July 10, 2014

Pawasa ageukia ukocha kwa nguvu zote

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BEKI wa zamani wa klabu ya Simba, Boniface Pawasa amesema kwamba ndoto zake sasa ni kuwa kocha wa Kimataifa, baada ya kustaafu kucheza soka la ushindani uwanjani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Pawasa alisema kwamba dhamira hiyo itatimia kwasababu ameshaweka mipango kabambe.

Alisema mara baada ya kustaafu kucheza soka, aliamua kuingia kwenye hatua hiyo ya kuwa kocha mwenye mafanikio makubwa.

“Mipango yangu mikubwa kwa sasa ni kuhakikisha kuwa nakuwa kocha, hivyo naamini kwa mikakati hii kila kitu kitakuwa sawa.

“Nimekuwa nikipangilia mipango hii kwasababu ndio malengo yangu makubwa kuhakikisha kuwa nakuwa kocha wa mpira wa miguu,” alisema Pawasa.

Pawasa ni miongoni mwa wachezaji wa soka waliokuwa na mafanikio makubwa katika soka la Tanzania, huku akiwika kwenye klabu ya Simba na timu ya Taifa (Taifa Stars).

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...