Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Kilindi, DC
Suleiman Liwowa, ameipongeza timu ya Tingisha FC kwa kuonyesha kiwango kizuri
katika mashindano ya Gallawa Cup yaliyofanyika jijini Tanga.
DC wa Wilaya Kilindi, Suleiman Liwowa, pichani.
Katika mashindano hayo, Tingisha FC
walifanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuwafunga ndugu zao Korogwe kwa
bao 3-1.
Akizungumza mwishoni mwa wiki, DC Liwowa
alisema kwamba vijana wake wa Kilindi wameonyesha kiwango cha aina yake na
kusisimua wengi katika mpira wa miguu.
Alisema kuwa anaamini vijana hao wataendelea
kufanya mazoezi ili kulinda viwango vyao na hatimaye kutafuta mafanikio zaidi
kwenye soka.
Mashindano ya Gallawa Cup
yaliandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa, maalumu kwa ajili ya
kujenga undugu mkoani humo.
“Timu yetu imefanikiwa kushika nafasi ya tatu, lakini
kiwango chake ni kizuri na hakika wilaya yangu imefarijika.
No comments:
Post a Comment