https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Friday, July 11, 2014

Vijana wa Skylight Band waendeleza makamuzi Thai Village

DSC_0034
Meneja wa Bendi Aneth Kushaba AK47 kwenye hisia kali wakati akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar huku Hashim Donode akipiga back vocal. TUKUTANE THAI VILLAGE LEO USIKU KUANZIA SAA TATU BILA KUKOSA.
DSC_0008
Digna Mbepera akiimba kwa hisia huku Aneth Kushaba AK47 akimpa sapoti.
DSC_0068
Divas watatu wa Skylight Band wakitoa burudani kwa mashabiki wao ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar Ijumaa iliyopita. Kutoka kushoto ni Digna Mbepera, Mary Lucos na Meneja wa Bendi Aneth Kushaba AK47.

DSC_0015
Mary Lucos binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka Pangoni akifanya yake jukwaani.
DSC_0138
Mashabiki wa Skylight Band mdogo mdogo wakijisogeza kwa dancing floor.
DSC_0044
Hashim Donode akilisongesha ndani ya kiota cha Thai Village Ijumaa iliyopita huku Mary Lucos akitoa sapoti ya back vocal.
DSC_0075
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo...Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo ...Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo...Joniko Flower akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akisindikizwa na mmoja wa Madiva wa Skylight Band Digna Mbepera.
DSC_0093
Agauuu.........Sebene ndio lishaanza hapo sasa....Sony Masamba na Sam Mapenzi wakionyesha ufundi wa kulisakata huku Joniko Flower akishuka mistari.
DSC_0097
Vijana machachari wanaotikisa jiji kwa sasa Skylight Band wakishambulia jukwaa ndani ya kiota cha Thai Village Masaki.
DSC_0105
DSC_0132
Sugua sugua mpaka kitake......Joniko Flower akishuka mistari huku Aneth Kushaba AK47, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakifanya kwa vitendo moja ya Style zinazobamba kwa mashabiki wa bendi hiyo.
DSC_0135
DSC_0229
Sugua sugua....JembeniJembe akiwasindikiza vijana wake pamoja na mashabiki ndani ya kiota cha maraha cha Thai Village Ijumaa iliyopita.
DSC_0195
Mashabiki nao waliitikia wito na kujaa kwenye dancing floor...uwapo Skylight Band huwezi kuboreka hata siku moja na wala kukaa chini ni lazima utatingisha mguu ama kuinuka na kucheza kama inavyoonekana pichani.
DSC_0170
Nipe Saluti.....x2 Kikosi kazi cha Skylight Band kikishambulia jukwaa.
DSC_0158
Shabiki wa Skylight Band anayetambulika kwa jina kisanii BAYO ABRAHAM aliyeshawahi kuvuma kwenye anga za muziki wa Bongo Flava akipagawisha jukwaani kwa kucheza Style mbalimbali za bendi hiyo Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village.
DSC_0165
JembeniJembe aliguswa na uchezaji wa BAYO na kwenda kumtunza.
DSC_0219
Mashabiki wa Skylight Band kwa raha zao wakisebeneka.
DSC_0233
DSC_0246
When Jesus say Yes, nobody can say No....When Jesus say Yes, nobody can say No....nayo inahusika pia si mwingine ni Aneth Kushaba AK47 akiwapa ladha tofauti mashabiki wa Skylight Band.
DSC_0247
DSC_0139
Mary Lucos na Digna Mbepera wakiwaangalia mashabiki wao(hawapo pichani) wanavyochizika na Bendi yao.
DSC_0189
Sam Mapenzi a.k.a asali ya warembo akifanya yake jukwaani.
DSC_0252
See gobe....Omo see gobe eh....See gobe...Omo see gobe eh....See gobe....Omo see gobe eh... Mashabiki wakichizika na Sam Mapenzi (hayupo pichani).
DSC_0271
Joniko Flower akipagawisha mashabiki na mduara.
DSC_0270
Mashabiki wakizungusha nyonga zao.
DSC_0273
Hapo sasa twende kazi mdogo mdogo.
DSC_0275
Kwa raha wadada kwa wakaka wakijimwaga kwa dancing floor.
DSC_0262
Mashabiki wa Skylight Band na Ukodak.
DSC_0047
Divas na Ukodak Back Stage....Mary Lucos na Digna Mbepera.
DSC_0215
Digna Mbepera na mmoja wa mashabiki wake wakipata Ukodak.
DSC_0106
Hakuna kama Skylight Band Wewe......!Mkurugenzi Mkuu wa Skylight Band JembeniJembe akipata Ukodak na Mary Lucos.
DSC_0085

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...