Na Mwandishi Wetu, Handeni
SEKESEKE la upangaji wa matokeo ya wanafunzi 138 wa sekondari
wilayani Handeni, mkoani Tanga, limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwa ni
kweli wanafunzi hao walisaidiwa na walimu wao katika Mtihani wa kidato cha nne.
Habari kutoka wilayani Handeni, mkoani Tanga, zinasema kuwa
wanafunzi hao wa shule za sekondari Kwaludege na Kwankonje, wamefutiwa matokeo
yao.
Uamuzi huo umetokana na Tume iliyoundwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Handeni, Dr Khalfany Haule, umebaini kuwa wanafunzi hao
walifanya udanganyifu kwenye mitihani yao kwa kusaidiwa na walimu wao.
Juzi Mkurugenzi wa Halmashuri ya wilaya ya Handeni Dk.
Halfany Haule alitoa majibu ya tume hiyo kuwa ni kweli wanafunzi hao walisaidia
katika mtihani.
Kwa mujibu wa matokeo ya Tume hiyo, serikali imeagizwa
kuchukua hatua stahiki dhidi ya walimu hao walioenda kinyume.
No comments:
Post a Comment