Na Kambi
Mbwana, Dar es Salaam
UONGOZI wa
klabu ya soka ya Coastal Union yenye maskani yake jijini Tanga, Tanzania
umesema kwamba hauwezi kuridhia kujiuzulu kwa Mwenyekiti wao Ahmed Aurora, kama
inavyodaiwa na baadhi ya wadau wa michezo kuwa mwenyekiti si za kweli.
Akizungumza
jana kwa njia ya simu, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Oscar Assenga, alisema kwa
Aurola bado ni mwenyekiti wao na hakuna mpango wowote wa kujiuzulu kama
inavyodaiwa na baadhi ya watu.
Alisema
kuwa mwenyekiti wao hana mpango wa kujiuzulu zaidi ya kuwa na fikra za kuijenga
klabu yao kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi ya Tanzania Bara
utakaoanza Septemba.
“Hakuna
mpango wowote wa kujiuzulu kwa mwenyekiti wetu, maana anachokifanya kwa sasa ni
kushirikiana na viongozi wenzake kwa ajili ya kuiongoza timu kwa mafanikio.
“Naamini
huu ni wakati muafaka kwa uongozi wetu kutulia na kuhakikisha kuwa Coastal
inakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ndani ya Tanga na nje pia, ukizingatia kuwa
ligi ijayo itakuwa na ushindani wa aina yake,” alisema.
Taarifa ya
kujiuzulu kwa Aurora zimekuja wakati ambao klabu hiyo bado haijatulia mara
baada ya Mkurugenzi wa Ufundi na aliyekuwa mdhamini wao Nassor BinSlum
kujiuzulu, sanjari na Msemaji wao Hafidh Kido.
No comments:
Post a Comment