Na Mwandishi Wetu,Tanga
AJALI iliyoangamiza roho za watu 10 katika kijiji cha Mbweni
Mkata, wilayani Handeni, mkoani Tanga, umetajwa kuwa chanzo cha ajali hiyo
iliyohusisha gari ya Ratco na Ngorika zilizogongana baada ya gari ndogo aina ya
Passo nayo kugongana na Ratco.
Hali ilivyoonekana katika ajali ya magari matatu ambayo ni Ratco, Ngorika na gari ndogo ya Passo
Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoani Tanga, Abdi
Issango, aliuambia mtandao wa Handeni Kwetu kuwa mwendo kasi ndio uliosababisha
ajali hiyo na kusababisha vifo vya watu 10, wakiwamo madereva wawili na abiria
wao nane.
Ajali hiyo ilitokea leo saa tano asubuhi ambapo awali Ratco
iligongana na Passo ambapo pia ikajumlisha na basi la Ngorika lililokuwa
linatoka Dar es Salaam kuelekea Arusha.
Majeruhi 35 katika ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali
ya wilaya Korogwe (Magunga), Handeni na ile ya Mkata kwa ajili ya kuwapatia
matibabu majeruhi hao.
No comments:
Post a Comment