Sasa barabara ya Msimbazi jijini Dar es Salaam inafungwa rasmi kuanzia leo Jumatano ya
01/04/2015.
Kikao Maalum kilichowahusisha Wadau mbalimbali Kutoka kwenye Taasisi za
Serikali kimekamilika punde na kukubaliana kufunga Rasmi Barabara ya
Msimbazi ifikapo saa sita usiku leo. Wadau waliohusika kama
inavyoonekana pichani ni pamoja na;
1. DART
2. Manispaa ya Kinondoni
3. Manispaa ya Ilala
4.
Halmashauri ya Jiji
5. SUMATRA
6. TANROADS
7. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
8. SMEC
9. STRABAG
10. JESHI LA POLISI.
Mabadiliko mbalimbali ni pamoja na kubadilika kwa mielekeo mbalimbali ya
Magari kutoruhusiwa kutumia barabara ya Msimbazi. Fuata maelekezo ya
viashiria mbalimbali ili kukuepushia usumbufu.
TUNAJENGA KWA AJILI YAKO TUNAOMBA USHIRIKIANO WAKO.
Tunaomba Taarifa hii uitume kwenye Makundi mengine au kwa Rafiki yako
ili kusaidia kusambaa kwa Taarifa hii muhimu kwa Wakazi wa Jiji la Dar
es salaam.
No comments:
Post a Comment