Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa tatu kushoto) akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (wa tatu kulia), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia), Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kuwasili kwenye mnuso wa uzinduzi wa mgahawa huo.(Picha zote na Zainul Mzige.
Na Mwandishi Maalumu, Trollhattan-Sweden
MGAHAWA mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania unaomilikiwa na mpishi maarufu duniani, Issa Kapande `Chef Issa’, umefunguliwa nchini Sweden na kuvunja rekodi ya dunia. Mgahawa huo ulizinduliwa na balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Balozi Msechu alimpongeza Issa Kapande na mkewe kwa kufanikisha kuwapo kwa mgahawa huo ambao umeweka rekodi kuwa mgahawa mkubwa kuliko yote ya Kiafrika katika nchi za Ulaya.
Aidha, alimshukuru Torvald Brahm mwenyeji wa mji huo kwa kumuunga mkono Issa hadi kufanikisha ndoto yake ya kuwa na mgahawa wa kwanza wa Kiafrika katika mji wa Trollhattan utakatoa huduma ya chakula cha kitanzania.
Katika uzinduzi huo ambapo wenyeji wa manispaa hiyo akiwemo Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund na msaidizi wake Peter Eriksson walikuwepo, balozi ambaye ndio kwanza ameanza kazi alielezea kufurahishwa na juhudi za Kapande.
Wadau wakiwa nje ya ukumbi tayari kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiwa na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) pamoja na Chef Issa Kapande (kulia) wakielekea kwenye eneo la tukio.
Alisema Issa ameonesha njia kwamba inawezekana kwa watu waliopo Ughaibuni sio tu kuajiriwa, bali kujiajiri katika nyanja mbalimbali.
Alisema hilo linawezekana kutokana na kufuatilia kwa karibu taratibu za wenyeji na kisha kutumia mafunzo yaliyopo kukamilisha ndoto.
"Ni dhahiri kuwa, Chef Issa kwa kupitia taaluma yake ya upishi amewezeshwa kumiliki mgahawa huu hapa Trollhattan,S weden kwa hilo, napenda tuishangilie na kuipigia makofi Sweden na Trollhattan."
Alisema akimpongeza kijana huyo ambaye pia amewekeza mkoani Mtwara.
Katika mahojiano, Mpishi Mkuu Issa Kapande alisema mafanikio yake yanatokana na juhudi kubwa na nia aliyoiweka katika kujifunza na kufundisha wengine katika mitandao ya wapishi wakuu.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago (kulia) wakielekea eneo la tukio.
Kapande ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya dhahabu katika upishi akiwa na timu ya Sweden magharibi alisema kuna umuhimu mkubwa kwa wapishi wa nyumbani kukubali kubadilika na kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo la kujifunza na kufunza ili kuwa na aina nyingine ya mapishi katika kuendeleza sekta.
Alisema akiwa amefanyakazi katika nchi 17 na tayari akiwa na vitega uchumi nchini alianzia nia ya kuwekeza Sweden mwaka 2009 wakati alipohamia nchini humo akitokea Uswisi. Alisema alianza kwa kuomba vibali, lakini mchakato kamili ulianza mwaka 2013.
"Tulilazimika kufanya utafiti kidogo" alisema na kuongeza kuwa katika utafiti huo walihoji watu 300 na kujua mwelekeo hasa wa shughuli yao unastahili kuwaje.
Kapande ambaye ni mhitimu wa chuo kikuu cha Manchester Metropolitan na Chuo kikuu cha kimataifa cha menejimenti ya hoteli cha Uswis amesema amepambana vikali na mkewe hadi kufikia hatua ya kuanzisha mgahawa huo ambao upo katika eneo la ukubwa wa skwea mita 810.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (wa pili kushoto) akikata utepe kuzindua rasmi mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande (wa pili kulia).
Wanaoshuhudia tukio hilo ni Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto), Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (katikati).
Ndani ya mgahawa huo pia watu mbalimbali watapatiwa taarifa za utalii Tanzania.
Katika kazi yake ya upishi, amebahatika kuwapikia watu mashuhuri duniani, baadhi wakiwa Andrew Young, Mchungaji Jesse Jackson, Robert Mugabe (Rais wa Zimbabwe), Paul Kagame (Rais wa Rwanda), Benjamini Mkapa (Rais mstaafu wa Tanzania), Raila Odinga (Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya), Daniel Arap Moi (Rais Mstaafu wa Kenya), Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi. Hillary Clinton na mumewe Bill Clinton, Mke wa Rais wa zamani wa Marekani Laura Bush.
Wengine ni Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, mwigizaji Chris Tucker, Rais wa zamani wa Afrika Kusini hayati Mzee Nelson Mandela, Koffie Olomide, Youssour ndour, Arsene Wenger (Kocha wa Arsenal ya England), Gianluca Vialli (nyota wa zamani wa Italia aliyewahi kuichezea na kuinoa Chelsea ya England), Rais wa Congo DRC, Joseph Kabila, Billy Gates na wengine wengi.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akiongozana na Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande kwenye sehemu maalum aliyoandaliwa.
Pichani juu na chini ni wadau kutoka kila kona ya dunia waishio nchini Sweden walihudhuria.
Bw. Per R. Bostrom akisalimiana na Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (aliyeketi). Kulia ni Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund wakiwa meza kuu.
Meza kuu.
Mwenyekiti wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo Kilumanga (katikati) akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa mgahawa huo.
Mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande akizungumza machache na wageni waalikwa kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kutoa risala ya ufunguzi.
Meza kuu wakifuatilia historia ya Chef Issa Kapande (hayupo pichani) wakati akizungumza na wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akisoma risala mara baada ya kuzindua mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden unaomilikiwa na mtanzania Chef Issa Kapande.
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago akitambulishwa kwa wageni waalikwa.
Baadhi wageni waalikwa wakisikiliza historia ya Chef Issa Kapande kabla ya mgeni rasmi kusoma risala ya ufunguzi.
Ukumbi mzima ulionekana kuvutiwa na historia ya maisha na mafanikio ya Mtanzania Chef Issa Kapande (hayupo pichani).
Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Chef Issa Kapande ambapo alimuomba aitafutie nafasi ndani ya mgahawa wake kama kumbukumbu.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu (kushoto) na mwenyeji wake Meya na mwenyekiti wa Trollhattan, Paul Akerlund pamoja na Makamu mwenyekiti wa kamati ya elimu wa Halmashauri ya Manispaa ya Trollhattans Stad, Fahime Nordborg (kulia) wakiongoza wageni waalikwa 300 kushiriki chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mmiliki wa mgahawa huo Chef, Issa Kapande.
Chef Issa Kapande akikata nyama ya Mbuzi kwa ajili ya mgeni rasmi, Mh, Balozi Dora Msechu.
Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mh. Dora Msechu akifurahi jambo na Meneja Mwendeshaji wa Kampuni ya Shamy Tours and Travel Agent Zanzibar, Khamis Mwinjuma Simba (kushoto).
Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund akijisevia minofu ya nyama ya Mbuzi wakati wa uzinduzi wa mgahawa huo.
Wageni wakiendelea kupakua chakula.
Mwenyekiti wa awali wa Chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Tengo Kilumanga (kulia) na mkewe wakishiriki chakula cha jioni kwenye mgahawa wa Mtanzania mwezao.
Katibu wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kushoto) pamoja na Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu ni miongoni kati ya wageni waalikwa 300 waliohudhuria uzinduzi huo.
Katibu wa Chama cha Watanzania Sweden (TANRIKS), Mathias Pembe (kulia), Mhasibu wa chama hicho, Bw. Emmanuel Ntundu (kushoto) pamoja na mtoto wa Mwenyekiti wa chama hicho, Grace Saulli wakijichana msosi uliondaliwa na Chef Issa Kapande.
Wageni waalikwa wakiendelea kupiga msosi uliofurahiwa na wengi ambao utakuwa unapatikana kwa chakula cha mchana kwa kipindi cha mwezi mmoja na hapo baadae itakuwa mpaka chakula cha usiku ndani ya mgahawa wa "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food).
Mh. Balozi Dora Msechu na mwenyeji wake Meya wa Trollhattan, Paul Akerlund.
Mgeni rasmi Mh. Balozi Dora Msechu kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa.
Mgeni rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa chama cha Watanzania waishio Sweden (TANRIKS), Daniel Saulli (kushoto), Mhasibu wa chama hicho, Emmanuel Ntundu (kulia), Katibu wa chama hicho, Mathias Pembe (wa pili kulia) pamoja na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
Mgeni rasmi Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mh. Dora Msechu (wa pili kulia) na Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha ya pamoja kikundi cha burudani.........
Mtanzania ambaye ni mmiliki wa mgahawa unaotoa huduma za chakula cha kitanzania unaofahamika kama "Lunch by Chef Issa" (The house of Tanzanian food) uliopo katika mji wa Trollhattan, Sweden, Chef Issa Kapande katika picha ya kumbukumbu na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago.
Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Tanzania, Tagie Daisy Mwakawago, Chef Issa Kapande katika picha ya pamoja na timu yake kwenye mgahawa huo.
Mdau Abraham Juma Ndwatta wa Ubalozi wa Tanzania nchini Sweden akiwa na Grace Saulli kwenye hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo.
Wadau wakiendelea kupiga picha na Mh. Balozi Dora Msechu.
Mh. Balozi Dora Msechu akisakata rhumba kwenye uzinduzi huo.
Chef Issa Kapande akicheza muziki na wageni waalikwa.
No comments:
Post a Comment