https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543

Recent Post

Wednesday, April 08, 2015

Angalia picha mbalimbali za Hitma ya kumuombea marehemu Mzee Abeid Amani Karume

Mama Fatma Karume akiwasili katika viwanja vya Afisdi Kuu ya CCM Kisiwandui kwa ajili ya kuhudhguria Hitma na dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Mjini Zanzibar.
Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume akiwaili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM kuhudhuria hitma ya Baba yake Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, iliofanyika leo Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM na kupokelewa kwa na Askari wa JWTZ , akihudhuria Hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. Afisi Kuu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai alipowasili katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kuhudhuria Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume iliofanyika leo.
Shekh Thabit Noman Jongo akitowa maelezo ya hafla ya kuaza kwa hitma na dua ya kumuombea Mzee Karume iliofanyika katika Afisi Kuu ya CCM kisiwandui Zanzibar. 
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi akisoma dua kabla ya kuaza kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.kilichofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. 
Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh. Saleh Omar Kabi akisoma dua kabla ya kuaza kwa kisomo cha hitma ya kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.kilichofanyika leo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.kulia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekh. Khamis Haji Khamis na kushoto Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume.

Viongozi wa Dini na Wananchi wakiwa katika ukumbi wa hafla wakiitikia Dua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika kisomo cha hitma kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kulia Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Kadhi Mkuu wa Zanzibar  Shekh. Khamis Haji Khamis, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe, Pandu Ameir Kificho.
Viongozi wakisoma hitma ya Marehemu Mzee Abeid Amani Karume wa kwanza Mufti Mkuu wa Zanzibar Sh. Saleh Omar Kabi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Othman Makungu.
Wananchi wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM wakimsomea kisomo cha Hitma Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Sh. Alhad Mussa akitowa mawaidha kwa Wananchi na Viongozi waliohudhuria kisomo cha Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Karume kilichofanyika katika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar leo.   
Viongozi wa Serekali na Dini wakimsikiliza Shekh wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Shekh. Alhad Mussa akitowa mawaidha baada ya kumaliza kusoma hitma na dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.wa kwanza Muftim Kuu wa Zanzibar Sh. Saleh Omar Kabi. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalif Seif Sharif Hamad, Rais Mstaaf wa Zanzibar Dk Amani Karume 
Viongozi wa Serekali na Dini wakimsikiliza Shekh wa Mkoa wa Dar-es-Salaam Shekh. Alhad Mussa akitowa mawaidha baada ya kumaliza kusoma hitma na dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karume. 
Mhe Mark Mwandosa akiwa makini akimsikiliza Mhe Bernard Membe wakiti wakihudhuria Hitma na Dua ya kumuombea Marehemu Mzee Abaid Amani Karume iliofanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi zao Zanzibar wakihudhuria hafla hiyo ya kisomo cha Hitma na Dua Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Mama Fatma Karume akiwa na Mke wa Rais Mstaafu wa Zanzibar  Dk Amani Karume na Mke wa Balozi Ali Karume, wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM wakihudhuria hitma na Dua ya kumuombea Mrehemu Mzee Abeid Amabni Karume ilofanyika leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Wake wa Viongozi wakihudhuria hitma na dua ya kumuombea Mzee Karume iliofanyika leo katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.
Walimu wa Madrasa wakihitimisha hitma kwa upande wa Wanawake waliohudhuria katika kisoma hicho Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
Wananchi wakiwa katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM wakimsomea kisomo cha Hitma Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Wanafunzi wa Madrasa Zanzibar wakihudhuria katika hafla hiyo ya kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu Mzee Abeid Amani Karum.

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...