https://tpc.googlesyndication.com/simgad/8045142562622600543


Recent Post

Thursday, April 02, 2015

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam aongoza upandaji miti Mabwepande wilayani Kinondoni

Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema waathirika wa mafuriko ya mto Msimbazi walioondoka baada ya kupewa viwanja maeneo ya Mabwepande na kurudi eneo la Msimbazi watanyang'anywa viwanja hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki ya upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofikia tamati jana kwa upandaji miti kwenye viwanja vya Shule ya Msingi ya Mji Mpya iliyopo Mabwepande ambapo Wilaya ya Kinondoni ilikuwa mwenyeji.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda akipanda mti katika maadhimisho hayo.
 Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi wengine wa Manispaa Kinondoni jinsi ya upandaji wa mimea mbalimbali pamoja na miti kwa kutumia matairi ya magari yaliyotumika.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa wamebeba miche ya miti wakielekea kuipanda katika maeneo mbalimbali shuleni hapo.
 Wananchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ya upandaji miti.
 Wanafunzi wa shule hiyo wakiwa kwenye sherehe hiyo.
 Msanii akitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni akipanda mti.
 Diwani wa Kata ya Mabwepande, Clement Bocco  akipanda mti katika eneo la shule ya Mji Mpya.
 Mratibu wa mazingira kutoka Taasisi ya EBPA, Charles Lugenga (kushoto), akimpatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki kikapu kilichotengenezwa kwa matairi yaliyotumika baada ya maadhimisho hayo.
 Wasanii wakitoa burudani.
 Maofisa wa Manispaa ya Kinondoni wakiwa kwenye 
maadhimisho hayo.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto), na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda wakiserebuka pamoja na wananchi katika maadhimisho hayo ya upandaji miti mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika leo viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande.
Wananchi wakicheza segere baada ya kumalizika kwa zoezi 
hilo la upandaji miti.

"Natoa maagizo kuwa wale wote waliopewa viwanja na serikali hapa Mabwepande ambao wameondoka viwanja vyao wanyang'anywe kwani ni wasariti na wale waliouziwa imekula kwao kwani serikali haiwatambui" alisema Sadiki.

Sadiki alitoa mwito kwa wananchi kubadilika kwa kuacha kutumia nishati ya miti na mkaa badala yake watumie gesi ambayo inapatikana kwa wingi kutokana na jitihada za serikali ili kulinda mazingira.

Aliongeza kuwa suala la upandaji miti ni endelevu hivyo kila mtu mahali alipo apande mti walau mmoja na kuitunza kwani miti ni uhai.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda alisema Manispaa hiyo inabustani kubwa  maeneo ya Kilongawima hivyo wanajipanga kuanzisha mashindano ya ukuzaji na upandaji wa miti kwa kata zake 34 na mshindi atapatiwa zawadi.

Katika hatua nyingine amesema halmshauri hiyo itawakopesha fedha wananchi waishio Mabwepande ambao waliathiriwa na mafuriko kwa ajili ya kukamilisha upatikanaji wa hati za umiliki wa viwanja vyao kabla ya mwezi wa sita badala ya kusubiri fedha kutoka ofisi ya Waziri Mkuu.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda alisema changamoto ya kukamilika kwa nyumba za askari polisi na kituo cha polisi katika eneo hilo itakwisha katika kipindi kifupi kijacho. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)

No comments:

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...