Basi linaloitwa Nganga Express likiteketea kwa moto mkoani Morogoro jana
Na Mwandishi Wetu, Morogoro
WIMBI la ajali nchini Tanzania linaendelea kutikisa, baada ya mkoani Morogoro watu 18 kudaiwa kufariki papo hapo jana asubuhi baada ya basi linaloitwa Nganga Express yenye namba za usajili T.373 BAH kugongana uso kwa uso na Mitsubish Fuso T.164 BKG maeneo ya Milima ya Udzunwa kando ya Mto Ruaha na basi hilo kuwaka moto, mkoani Morogoro.
Watu
wa karibu waliokuwa kwenye ajali hiyo walisema kwamba watu 15 walifariki kutoka
kwenye basin a wengine 3 kufariki kutoka kwenye fuso, ambapo majeruhi ni 10,
huku wanaume wakiwa 6 na wanawake 4.
Majeruhi
hao wamelazwa katika Hospitali ya St Kizito Mikumi na wengine wakilazwa katika
Hospitali ya Mtandika, mkoani Iringa. Katika ajali hiyo, pia inadaiwa kuwa
pikipiki moja iliteketea kwa moto na kuongeza kuwa inahisiwa pikipiki hiyo
ndiyo chanzo cha kuripuka kwa moto huo.
Wakati huo huo jana jioni iliripotiwa kuwa basi linalojulikana kama Burudani nusura liangamize roho za watu 50 baada ya kutaka kutumbukia mtaroni Soni, wilayani Lushoto
Wakati huo huo jana jioni iliripotiwa kuwa basi linalojulikana kama Burudani nusura liangamize roho za watu 50 baada ya kutaka kutumbukia mtaroni Soni, wilayani Lushoto
No comments:
Post a Comment